• HABARI MPYA

    Monday, March 26, 2012

    SIMBA WASHINDWA KUVUNJA REKODI YA MAPATO YA YANGA

    
    Omega Seme wa Yanga akichuana na mchezaji wa Zamalek
    MECHI ya kwanza ya Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) baina ya wenyeji Simba SC dhidi ya ES Setif ya Algeria Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana imeingiza kiasi cha Shilingi Millioni 268.
    Kwa mujibu wa taarifa kutoka Prime Time Promotions, waratibu wa mechi hiyo, jumla ya kiasi kilichopatikana ni Sh. 268, 539,000 kutokana na idadi ya tiketi za bei tofauti 43,592 zilizouzwa kwenye mchezo huo.
    Hata hivyo, mapato hayo hayafui dafu kwa mapato ya mechi ya kwanza ya Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Zamalek ya Misiri, ambayo iliingiza Sh 286, 695.000,00 mwezi uliopita.
    Lakini mapato hayo, yamezidi mapato ya mechi ya marudiano, Raundi ya kwanza Kombe la Shirikisho Afrika, kati ya Simba SC na Kiyovu ya Rwanda, ambayo yalikuwa ni Sh 208,843,000.00.
    Mechi zote hizo zilisimamiwa na Prime Time Promotions ya Dar es Salaam na zilichezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA WASHINDWA KUVUNJA REKODI YA MAPATO YA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top