• HABARI MPYA

    Saturday, March 24, 2012

    PEPE MCHAPA KIATU 'ATUPWA' JUKWAANI DAKIKA 180 LA LIGA

    Pepe kushoto akifanya viktu vyake vinavyomponza mara kwa mara. Hapa anamtandika teke Puyol wa Barcelona.
    BEKI mchapa kiatu wa Real Madrid, Pepe amefungiwa mechi mbili za Ligi Kuu ya Hispania, La Liga kwa kumtukana refa katika mechi waliyolazimishwa sare ya 1-1 Ijumaa na Villarreal.
    Mwenzake Sergio Ramos, hata hivyo aliponyoka adhabu kubwa baada ya adhabu ya kadi ya njano aliyoonyeshwa siku ya jumatano kupuuzwa na Kamati ya shirika la mpira la Uhispania.
    Beki huyu Mreno wa Real Madrid anaweza kucheza mechi ya leo na Real Sociedad.
    Kocha Jose Mourinho na kiungo Mjerumani, Mesut Ozil walionyeshwa kadi nyekundu wakati wa pambano hilo, baada ya Villarreal kupata bao la kusawazisha dakika za lala salam, nao wamefungiwa mechi moja kila mmoja.
    Kocha Msaidizi wa Mourinho, Rui Faria amefungiwa mechi mbili baada ya kutolewa nje katika kipindi cha pili Uwanja wa El Madrigal.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PEPE MCHAPA KIATU 'ATUPWA' JUKWAANI DAKIKA 180 LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top