• HABARI MPYA

    Friday, March 23, 2012

    MICHAEL JACKSON MFU ANAYEPIGA FEDHA NDEFU ILE MBAYA

    Michael Jackson enzi zake
    NI miaka miwili sasa tangu kufariki kwa Michael Jackson akiwa ana umri wa miaka 50, lakini Mfalme huyo wa Pop bado yuko kwa kuingiza fedha.
    Kwa mwaka wa pili mfululizo, Jackson anaongoza chati ya watu maarufu marehemu wanaoingiza fedha kibao (Top-Earning Dead Celebrities).
    Kwa miezi 12 iliyopita, Jackson ameingiza kiasi cha dola za Kimarekani Milioni 170 kutokana na mauzo ya muziki wake na hisa zake katika za Sony/ATV  Catalog.                                  Lakini Jacko ameporomoka ile mbaya, kutoka kiasi cha dola za Kimarekani Milioni 275 alizoingiza miezi 12 iliyotangulia, lakini bado inamuweka juu katika orodha ya marehemu maarufu wanaopiga pesa ndefu, akishika nafasi ya pili pia kwa ujumla kwa wafu na walio hai kwa kuingiza mkwanja mrefu, baada ya U2.W atu 15 katika orodha hii, wamevuna jumla ya dola Milioni 366 kati ya Oktoba 2010 na Oktoba 2011, ambayo inadhihirisha kifo si mwisho linapokuja suala la umaarufu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MICHAEL JACKSON MFU ANAYEPIGA FEDHA NDEFU ILE MBAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top