• HABARI MPYA

  Thursday, January 03, 2019

  MWADUI FC YAITANDIKA NDANDA 3-0 NA KUJIINUA KWENYE MSIMAMO WA LIGI

  Na Mwandishi Wetu, SHINYANGA
  TIMU ya Mwadui FC imeibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Ndanda FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mwadui Complex wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
  Ushindi huo umetokana na mabao ya washambuliaji wake, Ditram Nchimbi aliyefunga mawili dakika ya tisa na 18 na Frank Mbeshere dakika ya 83.
  Kwa ushindi huo, Mwadui FC inafikisha pointi 21 baada ya kucheza mechi zote 19 za mzunguko wa kwanza na kupanda hadi nafasi ya 12 kutoka ya 17.

  Ndanda FC inayobaki na pointi zake 19 baada ya kukamilisha mechi zake zote za 19 pia za mzunguko wa Ligi Kuu inaporomoka kwa nafasi moja hadi ya 17.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWADUI FC YAITANDIKA NDANDA 3-0 NA KUJIINUA KWENYE MSIMAMO WA LIGI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top