• HABARI MPYA

  Friday, January 04, 2019

  YANGA SC YAANZA VYEMA MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI, YAICHAPA KVZ 1-0

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  YANGA SC imeanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya KVZ usiku wa Alhamisi Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee dakika ya 78, kiungo Shaaban Mohamed akimalizia pasi ya mshambuliaji, Matheo Anthony Simon.
  Kwa ushindi huo, Yanga ilioyokuja na wachezaji wa kikosi cha pili kwenye mashindano haya wakiongezewa nguvu na nyota wachache wa kikosi cha kwanza, sasa inaongoza Kundi B kwa pointi zake tatu, ikifuatiwa na Azam FC, Jamhuri, KVZ na Malindi wenye pointi moja kila mmoja.
  Yanga watarejea dimbani Januari 5 kumenyana na Azam FC, kabla ya kuwavaa Malindi Januari 7 mechi zote zikianza Saa 2: 15 usiku na kumalizia na Jamhuri Januari 9 kuanzia saa 10:15 jioni.
    
  Michuano ya Kombe la Mapinduzi itaendelea kesho kwa mchezo kati ya Simba SC na Chipukizi kuanzia Saa 2:15 usiku, ambao utatanguliwa ne mechi kati ya Jamhuri na Malindi Saa 10:15 jioni.
  Kikosi cha KVZ kilikuwa; Yakoub Bakari Juma, Saleh Rajab Nassor, Makarani Miluchi Makarani, Iddi Mgeni Mrisho, Juma Abdallah Khamis, Othman Abdallah Ali/Masoud Abdallah Masoud, Suleiman Abdi Juma, Omar Hassan Khamis, Saloum Songoro Maulid/Feisal Riambi Lucas, Ayoub Lipati Kassim/Raphael Obi Mapunda na Mohamed Nassor Maulid/Suleiman Ali Suleiman.
  Yanga SC; Ibrahim Hamid, Yassin Saleh, Mwinyi Mngwali, Cleophas Sospeter, Said Juma ‘Makapu’, Maka Edward, Deus Kaseke, Gustavo Simon, Matheo Anthony/Salum Mkama, Erick Msagati/Pius Buswita na Shaaban Mohammed.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAANZA VYEMA MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI, YAICHAPA KVZ 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top