• HABARI MPYA

    Tuesday, January 01, 2019

    MANE, SALAH NA AUBAMEYANG WAINGIA FAINALI TUZO YA AFRIKA

    MWANASOKA Bora wa Afriaka, Mohamed Salah atetetea tuzo yake hiyo dhidi ya mchezaji mwenzake wa Liverpool, Sadio Mane na mshindi wa mwaka 2015, Pierre-Emerick Aubameyang.
    Kwa pamoja nyota hao watatu wanaocheza Ligi Kuu ya England wameingia fainali  ya tuzo ya Mwanasoka Bora wa Shirikisho la Kandanda Afrika (CAF) mwaka 2018.
    Watatu hao ambao ni marudio ya tatu bora ya msimu uliopita, kila mmoja atatumai kuuanza mwaka kwa ushindi wa tuzo hiyo ambayo itatolewa usiku wa Januari 8, mwaka 2019 mjini Dakar, Senegal.

    Nyota wa Gabon, Aubameyang, ameendelea kutokea katika tatu bora ya tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika tangu mwaka 2014, hii ikiwa mara ya tano kwake na kufikia rekodi ya gwiji wa Ivory Coast, Yaya Toure na kiungo wa Ghana, Michael Essien. 
    Mwanasoka Bora wa Mwaka Afrika mara nne, Toure, alifika fainali katika miaka ya 2011, 2012, 2013, 2014 na 2015 na Essien miaka ya 2005, 2006, 2007, 2008, 2009. 
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 sasa ana matumaini makubwa ya kunyanyua tuzo hiyo.
    Salah, mwenye umri wa miaka 26, aliweka historia baada ya kuwa Mmisri wa kwanza kushinda tuzo hiyo tangu ianzishwe mwaka 1992. 
    Ni mara ya pili anaingia fainali na Salah anataka kufikai rekodi ya wachezaji walioshinda mfululizo tuzo hiyo, Msenegal El Hadji Diouf (2001na 2002), Samuel Eto’o wa Cameroon (2003 na 2004) na Toure (2011 na 2012) ambao ni wachezaji pekee watatu kushinda tuzo hiyo mfululizo.
    Ni mara ya tatu kwa Mane mwenye umri wa miaka 26 kuingia tatu bora, akishika nafasi ya tatu mwaka 2016  na ya pili mwaka 2017. 
    Anatumai kuwa mchezaji wa tatu mwenye bahati na kuwa mchezaji wa pili tu wa Senegal kushinda tuzo hiyo baada ya Diouf.
    Kwa wanasoka Bora wa Mwaka wa Kike, walioingia fainali ni Wanigeria wawili Asisat Oshoala na Francisca Ordega na Chrestinah Thembi Kgatlana wa Afrika Kusini.
    Oshoala, mshindi wa tuzo mbili zilizopita ambaye kwa ujumla ameshinda tuzo tatu katika miaka ya 2014, 2016 na 2017 ana matumaini makubwa ya kushinda tuzo ya nne na kufikia rekodi ya mpinzani wake, Perpetua Nkwocha aliyeshinda 2004, 2005, 2010 na 2011. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MANE, SALAH NA AUBAMEYANG WAINGIA FAINALI TUZO YA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top