• HABARI MPYA

  Tuesday, January 01, 2019

  AMRI SAID AIACHA MBAO NA KUTUA BIASHARA UNITED INAYOSHIKA MKIA LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, MARA
  BEKI wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Amri Said ‘Stam’ amesaini mkataba wa miezi sita kumalizia msimu na klabu ya Biashara United ya Musoma mkoani Mara.
  Amri amesaini mkataba huo baada ya kuamua kuachana na Mbao FC ya mjini Mwanza kufuatia kutofautiana na uongozi wa klabu hiyo.
  Amri, beki wa zamani wa Maji Maji ya Songea na Simba SC ya Dar es Salaam anachukua nafasi ya Mrundi, Hitimana Thierry aliyeondolewa kutokana na matokeo mabaya Biashara United.

  Amri Said (kushoto) akisaini mkataba wa kujiunga na Mbao FC ya Musoma mkoani Mara

  Na ameondoka Mbao FC baada ya kukasirishwa na uongozi wa klabu hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Solly Zephania Njashi kumleta kocha mwingine, Ally Bushiri.
  Amri anaicha Mbao FC ikiwa katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara inayoshirikisha timu 20 baada ya kujiunga nayo Julai mwaka huu akitokea Lipuli FC ya Iringa.
  Lakini anaingia Biashara United ambayo inashika mkia kwenye Ligi Kuu ikiwa na pointi 10 baada ya kucheza mechi 16, nyuma ya Tanzania Prisons na African Lyon zenye pointi 12 baada y azote kucheza mechi 18.
  Amri sasa anakabiliwa na mtihani mkubwa wa kuinusuru Biashara United iliyopanda Ligi Kuu msimu huu kuteremka daraja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AMRI SAID AIACHA MBAO NA KUTUA BIASHARA UNITED INAYOSHIKA MKIA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top