• HABARI MPYA

  Wednesday, January 02, 2019

  FIFA YATEUA MAREFA WANNE TU TANZANIA KUCHEZESHA MECHI ZA KIMATAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limetuma orodha ya jumla ya marefa wa 18 wa Tanzania watakaochezesha mechi za kimataifa kwa mwaka 2019.
  Katika orodha hiyo ya marefa wenye beji za FIFA, waamuzi wakuu, yaani wapuliza kipyenga ni wanne tu upande wa wanaume, wakati sita ni waamuzi wasaidizi, maarufu kama washika vibendera.
  Katika orodha hiyo wapo waamuzi wa katikati na Waamuzi wasaidizi wa Kiume na wa Kikena waamuzi watakaochezesha mechi za soka la Ufukweni.

  Waamuzi wa katikati Wanaume ni Mfaume Ali Nassoro, Hery Ally Sasii, Emmanuel Alphonce Mwandembwa na Martin Elifhas Saanya, wakati Waamuzi Wasaidizi ni Ferdinand Chacha, Mgaza Ally Kinduli, Soud Iddi Lila, Frank John Komba, Mohamed Salim Mkono na Mbaraka Haule.
  Waamuzi wa kike wa Katikati, Jonesia Rukyaa Kabakama na Florentina Zabron Chief, wakati waamuzi wasaidizi wa kike ni Hellen Mduma Joseph, Grace Wamala, Janet Charles Balama na Mtwana Dalila Jafari na Waamuzi wa soka la Ufukweni ni Jackson Steven Msilombo na Geofrey Tumaini Mwamboneko.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FIFA YATEUA MAREFA WANNE TU TANZANIA KUCHEZESHA MECHI ZA KIMATAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top