• HABARI MPYA

  Tuesday, January 01, 2019

  ARSENAL YAZINDUKA, YAITANDIKA FULHAM 4-1 EMIRATES

  Washambuliaji wa Arsenal, Alexandre Lacazette na Pierre-Emerick Aubameyang wakishangilia kwa staili baada ya wote kufunga katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Fulham kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates.  Lacazette alifunga dakika ya 55 na Aubameyang dakika ya 83, wakati mabao mengine ya Arsenal yamefungwa na Granit Xhaka dakika ya 25 na Aaron Ramsey dakika ya 79 na la Fulham limefungwa na Aboubakar Kamara dakika ya 79.
  Kwa ushindi huo, ikitoka kupigwa 5-1 na Liverpool, Arsenal inafikisha pointi 41 baada ya kucheza mechi 21, ikiendelea kushika nafasi ya tano, nyuma ya Chelsea yenye pointi 43 za mechi 20 na mbele ya Manchester United yenye pointi 35 za mechi 20 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAZINDUKA, YAITANDIKA FULHAM 4-1 EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top