• HABARI MPYA

    Tuesday, September 19, 2017

    LIGI DARAJA LA PILI KUANZA SEPTEMBA 30

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    LIGI Daraja la Pili Tanzania Bara (SDL), inatarajiwa kuanza Septemba 30, mwaka huu kwa timu kuchuana katika viwanja vitano tofauti.
    Kwa mujibu wa Ratiba ambayo imeambatanishwa, michezo ya siku hiyo itakuwa ni kati ya Abajalo na Cosmopolitan; Namungo na Reha kutoka Kundi A wakati kundi B kutakuwa na mchezo kati ya Pepsi na Madini.
    Kundi C kutakuwa na mchezo kati ya Burkina
    Faso na Ihefu kadhalika Boma itacheza na Mkamba Rangers huku Kundi D likikutanisha timu za Bulyanhulu na Milambo.
    Katika Kundi hilo la D Mchezo kati ya Nyanza FC na Area C uliokuwa ufanyike Septemba 30, 2017 siku ya Jumamosi kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, sasa utachezwa Oktoba 01, 2017 siku ya Jumapili kwenye Uwanja huo huo.
    Sababu za mabadiliko haya ni kutokana na mchezo kati ya Pepsi FC vs Madini FC kuchezwa tarehe 30.09.2017 katika uwanja huo. Awali mchezo wa Nyanza na Area C ulipangwa kufanyika mkoani Manyara, lakini kutokana na hali ya uwanja ilibidi Bodi ya ligi ufanye mabadiliko husika. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIGI DARAJA LA PILI KUANZA SEPTEMBA 30 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top