• HABARI MPYA

    Saturday, June 06, 2015

    NIYONZIMA AITWA KIKOSI CHA 'NYIGU' KWA AJILI YA MAMBA LA MSUMBIJI

    Haruna Niyonzima ameitwa kikosi cha Rwanda kitakachoivaa Msumbiji wikiendi ijayo
    KIUNGO wa Yanga SC, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima amejumuishwa katika kikosi cha awali cha wachezaji 29 wa Rwanda maarufu kwa jina la Amavubi, yaani Nyigu kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Msumbiji.
    Kocha Mkuu wa Rwanda, Johnny McKinstry anatarajiwa kuwa na mtihani mzito mbele ya Msumbiji mchezo wa kufuzu AFCON ya mwaka 2017 wikiendi ya Juni 13 na 14 mjini Maputo.
    Kocha huyo pia amemuita Elias Uzamukunda anayecheza Ligi Daraja la kwanza Ufaransa katika klabu ya ASF Anderieux, na mchezaji wa Gor Mahia ya Kenya, Abouba Sibomana ambao wote wanatarajiwa kuingia kambini Jumatatu baada ya kumaliza majukumu ya klabu zao wikiendi hii.
    Wachezaji 13 kutoka kikosi cha U-23 wamejumuishwa kwenye kikosi hicho na McKinstry amesema wachezaji 12 wa APR Alhamisi jioni baada ya mchezo wa Kombe la Amani dhidi ya La Jeunesse.
    Kikosi kamili cha Amavubi ni makipa; Eric Ndayishimiye (Rayon Sports), Olivier Kwizera (APR), Emery Mvuyekure (Police), Marcel Nzarora (Police).
    Mabeki: Emery Bayisenge (APR), Ismael Nshutiyamagara (APR), Faustin Usengimana (Rayon Sports), Herve Rugwiro (APR), Michel Rusheshangoga (APR), Fitina Ombolenga (SC Kiyovu), Eric Rutanga (APR), Abouba Sibomana (Gor Mahia).
    Viungo: Haruna Niyonzima (Yanga SC), Jean Baptiste Mugiraneza (APR), Yannick Mukunzi (APR), Djihad Bizimana (Rayon Sports), Robert Ndatimana (Rayon Sports),  Kevin Muhire (Isonga), Andrew Buteera Jean Claude Iranzi (APR), Jean Marie Safari (Gicumbi), Dominique Savio Nshuti (Isonga), Jacques Tuyisenge (Police), Bertrand Iradukunda (APR).
    Washambuliaji: Michel Ndahinduka (APR), Isaie Songa (AS Kigali), Ernest Sugira (AS Kigali), Antoine Ndayishimiye (Gicumbi), Elias Uzamukunda (ASF Anderieux).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NIYONZIMA AITWA KIKOSI CHA 'NYIGU' KWA AJILI YA MAMBA LA MSUMBIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top