SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limetangaza kuwasimamisha kwa muda usiojulikana kujihusisha na soka Jean-Guy Blaise Mayolas (pichani kulia) na Badji Mombo Wantete.
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FECOFOOT) na Katibu Mkuu wake wanakabiliwa na tuhuma za kukiuka maadili.
Bodi hiyo ya soka duniani imesema Maofisa hao wawili wapo chini ya uchunguzi kwa tuhuma za kukiuka maadili.
Rais wa Tume ya Maadili ya Idara ya Upelelezi ya FIFA, Cornel Borbely na Mwenyekiti wa Kizimba, Hans-Joachim Eckert wameagiza, wawili hao wasiruhusiwe kujihusisha na shughuli zozote za soka kitaifa na kimataifa.
Adhabu hiyo inafuatia tuhuma mbalimbali za ukiukwaji wa maadili zinazowakabili wawili hao kwa mujibu wa taarifa.
Tuhuma za maadili zinazozungumziwa katika kipengele hicho ni pamoja na rushwa, mgongano wa kimaslahi, kupokea bakhshishi na kukutwa na hatia.

.png)
0 comments:
Post a Comment