• HABARI MPYA

    Sunday, June 07, 2015

    FC PLATINUM ‘KIROHO SWAAFI’ YABARIKI NGOMA KUTUA YANGA SC

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    FC Platinum ya Zimbabwe imesema kwamba wapo kwenye mazungumzo na Yanga SC ya Tanzania juu ya biashara ya mshambuliaji Donald Ngoma (pichani kulia).
    Msemaji wa FC Platinum, Chido Chizondo amesema mazungumzo yanaendelea baina ya pande hizo mbili kwa matumaini ya mwafaka kufikiwa.
    “Naweza kuthibitisha kwamba, Yanga imeonyesha nia ya kumchukua Donald Ngoma, mazungumzo yameanza lakini hakuna makubaliano yaliyofikiwa hadi sasa,” amesema Chizondo.
    Mshambuliaji tegemeo wa FC Platinum, Donald Ngoma yuko mbioni kutua kwa vigogo wa Tanzania, Yanga SC kutoka timu ya Zvishavane.
    Ngoma, ambaye Mkataba wake unamalizika Platinum mwishoni mwa msimu ujao, aliivutia Yanga wakati timu hizo zilipokutana katika mchezo wa 32 Bora Kombe la Shirikisho Afrika.
    Yanga iliitoa FC Platinum kwa jumla ya mabao 5-2, ikishinda 5-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kwenda kufungwa 1-0 Uwanja wa Mandava mjini Zvishavane.
    BIN ZUBEIRY inafahamu Yanga SC na Ngoma wamekwishamalizana na sasa kinachoendelea ni kumalizana na klabu yake.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FC PLATINUM ‘KIROHO SWAAFI’ YABARIKI NGOMA KUTUA YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top