MSENEGALI Sadio Mane amefunga hat-trick ya haraka zaidi katika historia ya Ligi Kuu ya England akitumia dakika mbili na sekunde 56, timu yake, Southampton ikiichapa mabao 6-1 Aston Villa
Winga huyo hatari kweli, alifunga mabao yake katika dakika za 12 na sekunde 22, dakika ya 13 na sekunde 46 na dakika ya 15 na sekunde 18.
Shane Long akafunga mabao mengine mawili na lingine moja akafunga Graziano Pelle akimalizia krosi ya Mane. Christian Benteke ndiye aliyefunga bao la kufutia machozi la Villa.
Sadio Mane akiwapigia makofi mashabiki baada ya kuvunjwa rekodi iliyowekwa na akina Robbie Fowler na Dwight Yorke PICHA ZAIDI GONGA HAPA



.png)
0 comments:
Post a Comment