• HABARI MPYA

    Saturday, May 16, 2015

    YANGA SC: RUKSA MCHEZAJI YEYOTE ANAYEPATA TIMU NJE KUONDOKA

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    YANGA SC imesema kwamba haitamzuia kuondoka mchezaji wake yeyote atakayepata timu nje, kikubwa ni taratibu kufuatwa.
    Aidha, Yanga imekanusha uvumi ulionea kuwa umemzuia mshambuliaji Simon Msuva kwenda kucheza soka nchini Afrika Kusini.
    Akizungumzia na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Yanga SC, Dk. Jonas Tiboroha amesema kwamba Yanga haijapata ofa yoyote inayomhusu Msuva ndo maana wamekuwa kimya.
    Amesema wanashangazwa na taarifa zilizoenea kuwa wamemzuia mfungaji huyo bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwenda kujiunga na Bidvest Wits ya Afrika Kusini.
    Simon Msuva hajazuiwa kwenda Bidvest

    “Kwanza napenda ifahamike Msuva alitoroka kwenda Afrika Kusini, wakati timu ikiendelea kucheza ligi na akijua wazi yeye bado ni mchezaji wa Yanga, kwani ana mkataba wa mwaka mmoja na nusu, hivyo nasema alijipeleka mwenyewe”, alisema Tiboroha.
    Aidha, Tiboroha amesema wao hawana kizuizi chochote cha kumuachia mchezaji yeyete kwenda kujaribiwa akipata ofa ambayo klabu au wakala wake watafuata taratibu, kwani wanajua atakapofuzu lazima klabu husika itawasiliana nao au wakishindwana wanafuata taratibi zingine ikiwa ni pamoja na kwenda FIFA.
    Tiboroha alisema mpaka sasa kuna mchezaji mmoja tu ambaye amewasilisha barua kwao ya kwenda kufanya majaribio na yupo tayari kumpa kibali, lakini hakumtaja.
    Amewataka wachezaji kuongeza thamani yao na utu kwa kusubiri kuitwa na si kujipeleka, kwani ndiyo maana wanapata ofa ndogo tofauti na thamani yao.
    Simon Msuva aliondoka kwenda kufanya majabio na klabu Bidvest Wits ya Afrika Kusini na amesharejea nchini na kujiunga na kambi ya timu ya Taifa ambayo nayo imekwenda kwenye mashindano ya COSAFA yanayoanza kesho nchini Afrika Kusini 
    Msuva alisajiliwa na Yanga misimu miwili iliyopita akitokea Moro United, amechukua tuzo ya ufungaji bora kwa mabao 17 aliyofunga.
    Endapo Msuva angefanikiwa kujiunga na Bidvest, angekuwa mchezaji wa pili wa kutegemewa na Yanga aliyeshiriki kikamilifu kuipa ubingwa msimu huu kuondoka kwani wa kwanza ni Mrisho Ngassa anayetimkia Free State Stars ya Afrika Kusini pia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC: RUKSA MCHEZAJI YEYOTE ANAYEPATA TIMU NJE KUONDOKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top