• HABARI MPYA

    Thursday, May 28, 2015

    NI NAMIBIA NA MSUMBIJI FAINALI KOMBE LA COSAFA 2015

    TIMU za taifa za Namibia na Msumbiji zitakutana katika fainali ya Kombe la COSAFA mwaka 2015 baada ya kushinda mechi zao za Nusu Fainali leo Uwanja wa Moruleng mjini Rusternburg, Afrika Kusini.
    Timu zote zilipata ushindi wa mbinde katika Nusu Fainaoi mbili ambazo jumla ya mabao manane yalitiwa nyavuni.
    Namibia imeifunga Madagascar mabao 3-2, shukrani kwake Paul Shalulile aliyefunga bao la ushindi zikiwa zimesalia dakika sita.
    Hadi mapumziko, timu hizo zilikuwa zimefungana mabao 2-2 mabao yote manne yakipatikana ndani ya 14 za kwanza kutokana na makosa ya safu za ulinzi.
    Benson Shilongo aliifugia mabao mawili Namibia, la kuongoza dakika ya 18 na la kusawazisha dakika ya 32 na sasa anaongoza kwa mabao katika michuano hiyo akifikisha manne.
    Naye Sarivahy Vombola aliinua idadi yake ya mabao katika mashindano hayo hadi kufika matatu baada ya kuifungia mabao mawili Madagascar.
    Nusu Fainali ya pili, Msumbiji waliifunga 2-1 Botswana. Isac Decarvalho alianza kuifungia Msumbiji dakika ya 65, kabla ya Omaatla Kebatho kuisawazishia Botsawna.  Luis Parkim aliyetokea benchi akaifungia bao la ushindi Msumbiji na kutinga fainali ya kwanza ya COSAFA tangu mwaka 2008.
    Kesho kutakuwa Fainali ya vibonde, maarufu kama michuano ya Plate, waliokuwa mabingwa watetezi, Zambia wakimenyana na Malawi Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace kuanzia Saa 11:00 jioni.
    Fainali ya COSAFA inatarajiwa kufanyika Jumamosi kati ya Namibia na Msumbiji Uwanja wa Moruleng kuanzia Saa 11:30 jiomi, wakati Botswana na Madagascar zitamenyana na Saa 9: 00 Alasiri kusaka mshindi wa tatu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NI NAMIBIA NA MSUMBIJI FAINALI KOMBE LA COSAFA 2015 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top