• HABARI MPYA

    Sunday, February 01, 2015

    EG YAING’OA TUNISIA ‘KIMAZABE’ NA KUTINGA NUSU FAINALI AFCON

    WENYEJI Equatorial Guinea wametoka nyuma kwa bao 1-0 na kushinda 2-1 dhidi ya Tunisia hivyo kufuzu Nusu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2015.
    Shukrani kwake, mfungaji wa mabao yote hayo mawili kwa mipira ya adhabu, Javier Balboa usiku huu mjini Bata katika mchezo uliodumu kwa dakika 120.
    Balboa alianza kufunga kwa penalti ya utata dakika ya 90 kusawazisha bao la Tunisia lililofungwa na Ahmed Akaichi dakika ya 70 na baadaye akafunga bao zuri kwa shuti la mpira wa adhabu nje kabisa ya boksi dakika ya 101 kuipatia Equatorial Guinea tiketi ya Nusu Fainali.

    Javier Balboa akishangilia baada ya kuifungia bao la pili EG

    Kwa matokeo hayo, EG itakutana na mshindi kati ya Ghana na Guinea zitakazomenyana Jumapili. Nusu Fainali hiyo ya pili, itapigwa mjini Malabo Alhamisi ya Februari 5.
    Katika mchezo wa kwanza, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ilitoka nyuma pia na kushinda 4-2 dhidi ya jirani zao, Kongo-Brazzaville mjini Bata na kutinga Nusu Fainali.
    Mabao mawili ya Dieudonne Mbokani yametosha kuwafanya Chui hao watinge Nusu Fainali kwa mara ya kwanza tangu 1998.
    DRC sasa inasubiri  mshindi wa mechi ya Jumapili kati ya Ivory Coast na Algeria ikutane naye katika Nusu Fainali Februari 4.
    Dakika 45 za kwanza zilimalizika bila bao leo, kabla ya mvua ya mabao kuanza kipindi cha pili, Dore February akiifungia bao la kwanza Kongo dakika ya 55 na Thievy Bifouma kufunga la pili dakika sita baadaye.
    DRC ilipata bao lake la kwanza dakika ya 65, mfungaji Mbokani kabla ya dakika 10 baaaye Jeremy Bokila kusawazisha. Joel Kimwaki akafunga bao la tatu dakika ya 80 kabla ya Mafoumbi kufunga la nne.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: EG YAING’OA TUNISIA ‘KIMAZABE’ NA KUTINGA NUSU FAINALI AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top