• HABARI MPYA

    Saturday, February 21, 2015

    RT WAJA NA MKAKATI MPYA WA KUIBUA VIPAJI VYA RIADHA NCHINI

    Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
    MAOFISA michezo na Maofisa Elimu wa mikoa ya Tanzania wameombwa kushirikiana na wenyeviti wa mchezo wa riadha kufufua mchezo huo kutoka ngazi ya shule za msingi na Sekondari.
    Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui akizungumza katika mkutano Mkuu wa Mwaka wa tathmini wa mashindano ya Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Shule za Sekondari (UMISETA) yanayosimamiwa na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)alisema imefika wakati kila mdau achangie kufufua mchezo huo.
    Alisema mchezo huo ambao zamani ulitangaza Tanzania katika mashindano mbalimbali duniani unazidi kupoteza umaarufu kwa sababu hakuna mikakati madhubuti ya kufuatilia wanamichezo wenye vipaji kutoka ngazi ya shule za msingi hadi vyuo vikuu.
    Nyambui alisema kwa mara ya mwisho mwaka jana Tanzania ilishiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika Scotland ikiwa ni baada ya miaka 40 kutoka na mchezaji Basil John mita 1500 kushika nafasi ya nane kati ya 12 walioingia fainali.

    Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui ameelezea mikakati ya kuibua vipaji vya wakimbiaji

    Alisema mchezo wa riadha hauna wafadhili kama ilivyo michezo ya soka lakini amejitahidi kushawishi kampuni ya Isere Sports isaidie kuwauzia wachezaji wa riadha vifaa kwa bei ya chini.
    "Tumekubaliana na Kampuni ya Isere Sports iagize na kuwauzia wetu vifaa vya michezo kwa bei ya kawaida ili wamudu kununua viatu na jezi za " alisema Nyambui.
    Meneja Masoko wa Isere Sports, Abbas Ally Isere alisema ni kweli wamefikia makubaliano hayo na yeye kama mtanzania anayehitaji vipaji vionekane atajitahidi kuhakikisha vifaa vya riadha anaviagiza na kuviuza kwa bei ya chini.
    Mikoa inayotamba kutoa wanariadha wengi ni Manyara, Arusha, Mara, Mtwara, Dodoma, Mbeya, Kanda ya Ziwa na mikoa nyingine.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RT WAJA NA MKAKATI MPYA WA KUIBUA VIPAJI VYA RIADHA NCHINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top