• HABARI MPYA

  Sunday, February 01, 2015

  WACHEZAJI SIMBA SC WAMPA ZAWADI YA ‘BETHIDEI’ KOCHA WAO KOPUNOVIC

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  NAHODHA wa Simba SC, Hassan Isihaka amesema kwamba ushindi wao dhidi ya JKT Ruvu Jumamosi ni zawadi kwa kocha wao, Goran Kopunovic ambaye Jumapili anasherehekea kuzaliwa kwake.  
  Simba SC iliifunga mabao 2-1 JKT Ruvu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumamosi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Jumapili Mserbia, Kopunovic atakuwa anatimiza miaka 48 tangu azaliwe Februari 1, mwaka 1967.
  “Tumefurahi kupata ushindi huu na hii ni zawadi nzuri kwa kocha wetu (Goran) ambaye anasherehekea siku yake ya kuzaliwa,”alisema Isihaka.
  Kocha Goran Kopunovic anatimiza miaka 38 tangu azaliwe na wachezaji wake wamempa zawadi ya ushindi asherekee vizuri siku yake hiyo muhimu

  Mabao mawili ya mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Dan Sserunkuma jioni ya jana yalituliza hali ya hewa Msimbazi, baada ya Simba SC kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya JKT Ruvu.
  Hamkani ilianza kuwa si shwari ndani ya Simba SC, baada ya kipigo cha mabao 2-1 pia katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu mbele ya Mbeya City Uwanja wa Taifa, lakini Sserunkuma ameweka mambo sawa jana.
  Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Ofisa wa jeshi la Polisi, Hashim Abdallah wa Dar es Salaam, aliyesaidiwa na Rashid Zongo wa Iringa na Abdallah Shaka wa Tabora, hadi mapumziko kila timu ilikuwa imekwishapata bao moja.
  Dan Sserunkuma (wa pili kushoto) alifunga mabao yote mawili katika ushindi huo

  Simba SC ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Dan Sserunkuma, aliyemaliza pasi ya Mganda mwenzake, Emmanuel Okwi kutokea pembeni kulia.
  JKT Ruvu walisawazisha bao hilo kupitia kwa George Minja dakika ya 19 aliyeunganisha kwa kichwa kona ya Jabir Aziz.
  Kipindi cha pili, Simba SC ilikianza vizuri na dakika ya pili tu, Sserunkuma tena kwa usaidizi mzuri wa Okwi akaipatia timu yake bao la pili ambalo linakuwa Bao lake la tatu katika ligi tangu asajiliwe Desemba kutoka Gor Mahia ya Kenya.
  Na ushindi huo umekuwa zawadi nzuri kwa kocha Mserbia, Goran Kopunovic akisherehekea siku ya kuzaliwa kwake Jumapili. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WACHEZAJI SIMBA SC WAMPA ZAWADI YA ‘BETHIDEI’ KOCHA WAO KOPUNOVIC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top