• HABARI MPYA

    Thursday, February 26, 2015

    MALINZI AMLILIA REFA ALIYEFARIKI DUNIA

    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amepeleka salamu za rambirambi kwa familia ya mwamuzi mstaafu Mohamed Nyama ambaye pia aliwahi kuwa mjumbe wa kamati ya waamuzi  ya TFF kilichotokea jana kwao Nachingwea- Lindi.
    Marehemu Mohamed Nyama wakati wa uhai wake alikuwa mwamuzi wa daraja la kwanza ambaye pia alitambuliwa na FIFA, Nyama anatarajiwa kuzikwa leo jioni kwao Nachingwea mkoani Lindi na TFF itawakilishwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Bw. Athumani Kambi.
    Katika salam zake kwa familia ya Nyama, kwa niaba ya TFF, familia ya mpira wa miguu na watanzania Rais Malinzi amewapa pole wapenzi wa mpira wa miguu nchini  katika kipindi hiki kigumu cha maombelezo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALINZI AMLILIA REFA ALIYEFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top