• HABARI MPYA

    Wednesday, February 18, 2015

    RED ARROWS KUJIPIMA NA KILUVYA UNITED, RUVU SHOOTING

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    TIMU ya Red Arrows inayoshiriki Ligi Kuu nchini Zambia, kesho siku ya alhamis itashuka uwanja wa Karume kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Kiluvya United inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL) Tanzania bara.
    Mchezo huo wa kirafiki ni sehemu ya maandalizi ya timu hiyo kutoka nchini Zambia ambayo imeweka kambi jijini Dar es salaam kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu nchini Zambia.
    Mara baada ya mchezo huo, Kikosi cha Red Arrows kitaendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Karume na Ufukwe wa Mbalamwezi kulingana na ratiba ya kocha wa timu hiyo.
    Kikosi cha Ruvu Shooting kitamenyana na Red Arrows ya Zambia

    Red Arrows watacheza mchezo wao wa pili na mwisho wa kirafiki siku ya jumapili dhidi ya timu ya Ruvu Shooting inayoshiriki Ligi Kuu (VPL), mchezo ambao utachezwa kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es salaam kabla ya kumaliza ziara yao siku ya jumanne na kurejea nchini Zambia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RED ARROWS KUJIPIMA NA KILUVYA UNITED, RUVU SHOOTING Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top