
KLABU ya Arsenal imetolewa kiume katika Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu baada ya kushinda 2-0 ugenini dhidi ya Bayern Munich nchini Ujerumani.
Matokeo hayo yanamaanisha matokeo ya jumla ni 3-3 baada ya awali, Bayern kushinda 3-1 Jijini London.
Bayern imesonga mbele kwa faida ya mabao ya ugenini na sasa imejikita Robo Fainali.
Olivier Giroud aliifungia Arsenal bao la kwanza dakika ya tatu ambalo lilidumu hadi mapumziko.
Laurent Koscielny akaja kuwafungia la pili The Gunners dakika ya 86, lakini Bayern wakabebwa na mabao yao ya ugenini kusonga mbele.
VIKOSI;
Bayern Munich: Neuer, Dante, Van Buyten, Lahm, Martinez, Muller, Alaba, Dias, Kroos/Tymoschuk dk81, Mandzukic/Gomez dk73, Robben
Benchi: Tom Starke, Rafinha, Contento, Shaqiri, Pizarro
Kadi za njano: Lahm, Martinez, Gomez
Arsenal: Fabianski, Mertesacker, Koscielny, Jenkinson, Gibbs, Rosicky, Arteta, Walcott/Oxlade-Chamberlain dk72, Ramsey/Gervinho dk72, Cazorla, Giroud
Benchi: Mannone, Vermaelen, Diaby, Coquelin, Arshavin
Kadi za njano: Gibbs, Rosicky, Giroud, Mertesacker, Cazorla, Koscielny
Wafungaji wa mabao: Giroud dk3 na Koscielny dk86
Refa: Pavel Kralovec
Mahudhurio: 66,000

Laurent Koscielny akifunga bao la pili kwa kichwa dakika za mwishoni

Kipa wa Bayern Munich, Manuel Neuer akiuzuia mpira dhidi ya wachezaji wa Arsenal baada ya kufungwa bao la pili, ili kupoteza muda

Olivier Giroud akifunga bao la mapema lililowatia presha wenyeji

Thomas Rosicky akionekana mwenye hasira baada ya kupewa kadi ya njano kwa kumchezea rafu Arjen Robben

Javi Martinez (kulia) akiondosha mpira miguuni mwa Mikel Arteta.

Mario Mandzukic akilalamikia uamuzi wa refa

Arsene Wenger akizozana na refa wa akiba

Wenger akikaribia mstari wa kuingia uwanjani huku akilalamikia uamuzi wa refa.

Luis Gustavo (kulia) akijaribu kumdhibiti Santi Cazorla

Thomas Muller akimbwatukia mshika kibendera

Arjen Robben akienda chini baada ya kupitiwa na kwanja la Kieran Gibbs


.png)