• HABARI MPYA

    Sunday, March 17, 2013

    AZAM FC HUREEEEE, YAUA 2-1 UGENINI STERLING SEIF ABDALLAH KARIHE

    Hongrea Azam FC

    Na Princess Asia
    AZAM FC imeanza vyema Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF), baada ya usiku huu kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji Barrack Young Controllers katika mchezo wa kwanza wa hatua hiyo uliofanyika kwenye Uwanja wa Antonette Tubman Monrovia, Liberia.
    Kwa matokeo hayo, Azam sasa itahitaji hata sare tu ili kusonga mbele, Raundi ya Tatu na ya mwisho ya mchujo kabla ya hatua ya makundi.
    Shujaa wa Azam FC leo alikuwa ni Seif Abdallah Karihe aliyefunga bao la ushindi dakika ya 90, kufuatia kazi nzuri ya Khamis Mcha ‘Vialli’.
    Katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Farouk Mohamed kutoka Misri, hadi mapumzikko, B.Y.C. walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililofungwa na Junior Barshall dakika ya 44.
    Azam wangeweza kuondoka uwanjani baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza wakiwa wana mabao, kama wangeweza kutumia nafasi nzuri takriban sita walizopata.
    Seif Abdallah; Shujaa wa Azam leo
    Kwa muda mrefu kipindi cha kwanza, B.Y.C. walikuwa wanacheza kwa kujihami zaidi wakiwategeshea mitego ya kuotea wachezaji wa Azam FC.
    Kipindi cha pili Azam FC baada ya kupata mawaidha ya kocha wao, Muingereza Stewart Hall walirejea uwanjani wamebadilika na kufanikiwa kusawazisha bao.
    Alikuwa ni kiungo wa kimataifa wa Kenya, Humphrey Mieno aliyeifungia bao la kusawazisha Azam FC.
    Azam inatarajiwa kurejea nchini kesho na mchezo wa marudiano utafanyika wiki mbili zijazo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Katika mchezo huo, kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Waziri Salum, David Mwantika, Joackins Atudo, Ibrahim Mwaipopo/Abdi Kassim ‘Babbi’ dk68, Humphrey Mieno, Kipre Balou, Khamis Mcha ‘Vialli’, John Bocco ‘Adebayor’/Jabir Aziz dk85 na Kipre Tcheche/Seif Abdallah dk80.
    Benchi; Aishi Manula, Luckson Kakolaki, Malika Ndeule, Abdulhalim Humud na Jabir Aziz.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: AZAM FC HUREEEEE, YAUA 2-1 UGENINI STERLING SEIF ABDALLAH KARIHE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top