• HABARI MPYA

    Wednesday, February 27, 2013

    RONALDO SHUJAAAAA, AMPOTEZA VIBAYA VIBAYA MESSI REAL IKIICHAPA 3-1 BARCA CAMP NOU

    NYOTA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ametoa majibu mazuri kwa wale wanaosema Leo Messi ni mchezaji bora wa dunia, kwa kufunga mabao mawili na kuipa timu yake ushindi wa 3-1 katika Nusu Fainali ya Kombe la Mfalme dhidi ya Barcelona.
    Na kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson alikuwapo kwenye Uwanja wa Nou Camp kuona kikosi cha Jose Mourinho kikishinda mchezo huo wa marudiano baada ya kuanza na sare ya 1-1 nyumbani— kitu ambacho Real inatumai kukifanya pia katika Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Old Trafford Jumanne ijayo.
    Huo ulikuwa usiku babu kubwa kwa Mourinho ndani ya Barcelona tangu aiwezeshe Inter Milan kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa akiwa na wachezaji 10.
    Star: Cristiano Ronaldo scored two goals as Real Madrid beat Barcelona 3-1 at the Nou Camp
    Nyota: Cristiano Ronaldo alifunga mabao mawili Real Madrid ikiifunga Barcelona 3-1 Uwanja wa Nou Camp

    TAKWIMU ZA MECHI

    Barcelona: Pinto, Alves, Pique, Puyol, Jordi Alba, Sergio, Xavi (Alcantara 74), Cesc (Villa 60), Pedro (Tello 71), Iniesta, Messi.
    Benchi: Valdes, Mascherano, Adriano, Song.
    Mfungaji: Alba dk89.

    Real Madrid: Diego Lopez, Varane, Ramos, Coentrao, Khedira, Cristiano Ronaldo, Ozil (Pepe 79), Xabi Alonso (Essien 84), Arbeloa, Higuain (Callejon 70), Di Maria.
    Benchi: Adan,Kaka, Benzema, Modric.
    Wafungaji: Ronaldo dk 13 na 57, Varane dk 68.
    Mashabiki: 90,002.
    Refa: Undiano Mallenco.
    Na ilikuwa mechi ambayo mrithi wa kocha aliyeondoka Barca, Pep Guardiola,Tito Vilanova alitaka kuanzisha zama mpya za ubabe wao kwa Real, lakini Ronaldo alizima hilo.
    Alimkimbiza Gerard Pique dakika ya 13 hadi akamchezea rafu kwenye eneo la hatari, wakati anamlamba chenga na akaenda kupiga mwenyewe hiyo penalti akimtungua kipa  Manuel Pinto na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee kufunga katika mechi sita za Clasico.
    Katika kipindi cha pili, wakati Barcelona wakitawala mchezo, Angel Di Maria alimtoka Carles Puyol katika shambulizi lingine la kushitukiza na alipopiga mira ukarudishwa, ukamkuta  Ronaldo, mshambuliaji wa zamani wa Manchester United tena, akiweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao mawili ugenini katika Clasico.
    Katika mchezo huo, Messi, ambaye aliingia uwanjani kusaka bao la 50 msimu huu, alifunikwa kama ilivyokuwa kwenye mechi na AC Milan.
    Cynical: Ronaldo was brought down by Gerard Pique in the penalty area in the 13th minute
    Ronaldo akiangushwa chini na Gerard Pique na kuwa penalti akaenda kufunga mwenyewe dakika ya 13
    Lead: Ronaldo sent Jose Manuel Pinto the wrong way to open the scoring from the spot
    Ronaldo akimpeleka kulia Jose Manuel Pinto, huku mpira ukitinga kushoto
    Ronaldo
    Cristiano Ronaldo
    Shujaa: Nyota wa Ureno akishangilia

    Messi alifunikwa na beki kinda Mfaransa, Raphael Varane, na alikuwa bwana mdogo huyo huyo wa miaka 19 aliyefunga kwa kichwa bao la tatu. 
    Bao la Varane lilikumbushia bao lake la kusawazisha katika mchezo wa kwanza na lilimsisimua mno Mourinho, ambaye alimvaa beki huyo wa kati kwenye mstari wa kuingia uwanjani na kuanza kushangilia naye.
    Jordi Alba aliifungia bao la kufutia machozi Barca dakika za lala salama akimalizia pasi nzuri ya Andres Iniesta.
    Gap: Ronaldo followed up Sami Khedira's effort to double Madrid's lead in the second half
    Ronaldo akifunga la pili
    Gap: Ronaldo followed up Sami Khedira's effort to double Madrid's lead in the second half
    Mourinho alimpeleka nje Iker Casillas kukutana na vyombo vya habari mwishoni mwa mchezo na kuitaka Real Madrid ihakikishe Ronaldo anabaki.
    Tetesi zinamhusisha mchezaji huyo na kurejea England, huku ikisemekana klabu hiyo haina mpango wa kumuongezea mkataba wake ambao unamalizika mwaka 2015, na Casillas alisema: ‘Ni mchezaji wetu muhimu mno katika mechi hizi kubwa.
    ‘Alikuwa tu siyo babu kubwa usiku huu, lakini amekuwa hivyo katika Clasicos nyingine. Ni shujaa wetu.’
    Cruising: Raphael Varane rose highest to head home from a corner and put Real 3-0 up
    Raphael Varane akifungwa kwa kichwa bao la tatu
    Delight: Varane celebrated his goal with manager Jose Mourinho 
    Delight: Varane celebrated his goal with manager Jose Mourinho
    Varane akishangilia bao lake na kocha Jose Mourinho
    Downbeat: Lionel Messi looked dejected as Madrid cruised past Barcelona
    Lionel Messi na chini kulia taabani
    Lionel Messi
    Too little, too late: Jordi Alba scored a late consolation for Barcelona
    Jordi Alba akishangilia bao lake la kufutia machozi
    Heated: Pepe fell to the floor as tensions ran high between the arch rivals
    Pepe akiwa ameanguka chini baada ya kupambana na wapinzani wake
    Scouting: Sir Alex Ferguson and his United assistant Mike Phelan were in the stands at the Nou Camp
    Sir Alex Ferguson na Msaidizi wake, Mike Phelan walikuwa Nou Camp jana
    Opposition: Mourinho talked to Barcelona's assistant coach Jordi Roura before the match
    Mourinho akizungumza na kocha Msaidizi wa Barcelona, Jordi Roura kabla ya mechi 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: RONALDO SHUJAAAAA, AMPOTEZA VIBAYA VIBAYA MESSI REAL IKIICHAPA 3-1 BARCA CAMP NOU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top