Beki wa timu ya soka ya Azam FC, Erasto Nyoni anayetumikia
adhabu ya kusimamishwa kwa muda usiojulikana na klabu yake, kwa tuhuma za
kuhusika kuihujumu timu hiyo katika mechi dhidi ya Simba SC, mzunguko wa kwanza
wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Picha hii ilipigwa jana wakati wa sherehe za Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL), wadhamini wa timu ya taifa, Taifa Stars kukabidhi basi la timu
hiyo, makao makuu ya kiwanda cha kampuni hiyo, Ilala, Dar es Salaam.
Nyoni ambaye amekumbwa na adhabu hiyo kwa pamoja na kipa Deo
Munishi ‘Dida’ na mabeki wenzake, Aggrey Morris na Said Mourad, aliwawakilisha
wachezaji wenzake wa Taifa Stars jana, ambao kwa kipindi hiki wamebanwa na
majukumu ya klabu zao.
Tazama mara mbili sura yake, je unaweza kukubali huyu jamaa
alicheza mchezo huo mchafu, au jumba bovu tu lilimdondokea?
|