• HABARI MPYA

    Wednesday, February 20, 2013

    KING DROGBA AREJEA LIGI YA MABINGWA USIKU WA LEO


    DIDIER Drogba anatarajia kukutana tena na rafiki zake wa zamani. Miezi tisa tangu afunge penalti ya ushindi pale Munich, amerudi tena kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, akiwa na matumaini ya kufanya maajabu mengine kwenye klabu yake mpya ya Galatasaray dhidi ya Schalke.
    Mchango wake mkubwa wakati wa harakati za Chelsea kutawala Ulaya, zilifikia keleleni Allianz Arena Mei mwaka jana, pale alipofunga bao la kusawazisha katika dakika ya 88 na kukosa penalty iliyookolewa katika muda wa nyongeza kabla ya kufunga penalty ya mwisho iliyoamua bingwa.

    Main man: Didier Drogba made a flying start to his career at Galatasaray with a goal five minutes into his debut
    Didier Drogba alianza maisha yake ya soka Galatasaray kwa kasi akifunga bao dakika ya tano tu ya mechi yake ya kwanza.

    Main man: Didier Drogba made a flying start to his career at Galatasaray with a goal five minutes into his debut

    JE, DROGBA ATAFANYA VIZURI?

    Muafrika wa Kwanza kufunga mabao 100, Ligi Kuu ya England
    Mchezaji pekee kufunga kwenye fainali nne za Kombe la FA
    Mfungaji Bora wa Kombe la UEFA, 2003-4
    Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya England 2007, 2010
    Timu Bora ya UEFA, 2007
    Timu Bora ya FIFA/FIFPRO, 2007
    Aliisaidia Chelsea kushinda Mataji yao mawili mfululizo ya kwanza
    Aliiongoza Ivory Coast kushiriki Kombe la Dunia kwa Mara ya kwanza mwaka 2006 nchini Ujerumani.
    Alifunga bao la kwanza la Ivory Coast kwenye Kombe la Dunia
    Mchezaji Bora wa Afrika, 2006, 2009
    Baada ya kuchukua Ubingwa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Drogba aliongea na Kombe, akiliuliza kwa nini limekuwa likimkwepa kwa muda mrefu, Jambo ambalo liliwashangaza wengi. “Lilikuwa kama tukio la Kidini,” alisema Mwenyekiti wa Chelsea, Bruce Buck. 
    Ujio wa Drogba Istanbul lilikuwa tukio ambalo liliwavuta wengi.
    Maelfu ya watu waliajaza Uwanja wa ndege wakilitaja Jina lake, wakiwasha mafataki, mamia waliujaza uwanja wa mazoezi kumuangalia siku ya kwanza akifanya mazoezi.
    Usajili wake ulikuwa wa pili wa mchezaji mwenye jina kubwa ndani ya mwezi mmoja katika klabu hiyo akifuata nyayo za Wesley Sneijder aliyetua kwenye klabu hiyo kwa ada ya pauni milioni 7, akitokea Inter Milan, Mholanzi huyo anaangalia uwezekano wa kufuata nyayo za Gheorghe Hagi katika klabu ya Galatasaray. 
    Lakini alikuwa ni Drogba ambaye alianza kwa kasi kwenye klabu hiyo akifunga bao la kichwa wakati timu hiyo iliposhinda kwa mabao 2-1 dhiodi ya Akhisar Belediye, alifunga bao hilo ikiwa ni dakika tano tu tangu aingie uwanjani akitokea benchi kucheza mechi yake ya kwanza. 

    Head boy: Drogba rose highest to score Chelsea's equaliser in Munich last May
    Goli: Drogba akiifungia Chelsea bao la kusawazisha jijini, Munich Mei mwaka jana.
    On the spot: Drogba also scored the winning penalty to complete Chelsea's stunning European triumph
    Ushindi: Drogba pia alifunga penalti ya ushindi na kuipa Chelsea Ubingwa wa Ulaya.
    End of an era: Drogba with the Champions League trophy after Chelsea's win over Bayern Munich
    Kamaliza: Drogba akiwa na taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya Chelsea kushinda fainali dhidi ya Bayern Munich

    MASHINE YA MABAO YA CHELSEA

    Drogba alifunga mabao 157, katika mechi 341 alizoichezea klabu hiyo na kumfanya kuwa mfungaji bora wa nne wa muda wote wa klabu hiyo.
    Mabao yake 34 kwenye michuano ya Ulaya ni Rekodi ya klabu kwa mabao 10.
    Amefunga mabao tisa kwenye mechi tisa za fainali.
    “Ni changamoto mpya, sehemu mpya ya maisha yangu,” alisema Drogba. Aliwaambia marafiki zake kwamba baada ya kuamua kuhama Shanghai Shenhua ya China chaguo lake la kwanza ilikuwa kuchezea klabu inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.
    Kwa Drogba, (34), lilikuwa swali la kuutumia vizuri mwaka wake wa mwisho kama mchezaji. FIFA walimuunga mkono kuhama licha ya viongozi wa Shanghai, Kugoma. Wiki iliyopita alipewa Leseni ya kuchezea Galatasaray na Kamati ya Hadhi ya Wachezaji ya FIFA, wakati akisubiri kumalizika kwa utata wa mkataba wake.
    Wakati Drogba akijiandaa kusikia kelele za mashabiki watakaokuwepo kwenye uwanja wa Turk Telekom Arena, wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 50,000, uwanja ambao umechukua nafasi ya ule wa Ali Sami Yen ambao pia ulikuwa na kelele kibao, atakuwa akijaribu kuongeza mabao kati ya yale 39 aliyonayo sasa kati ya mechi 77 za Ligi ya Mabingwa Ulaya.
    Schalke, wanatakiwa kuwa na tahadhari. Lolote linaweza kutokea wakati Drogba na washikaji zake wa zamani wanapokuwa pamoja kwenye mechi za Ulaya.

    Cauldron: Drogba can expect to be welcomed by a passionate home crowd on Wednesday night
    Mashabiki: Drogba anatarajia mapokezi makubwa leo usiku.
    Cauldron: Drogba can expect to be welcomed by a passionate home crowd on Wednesday night

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: KING DROGBA AREJEA LIGI YA MABINGWA USIKU WA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top