• HABARI MPYA

    Friday, February 22, 2013

    HASHIM KUCHEZESHA YANGA NA AZAM KESHO, KIBENDERA CHANG'WALU NA KANYEYE

    Wachezaji wa Azam
    Na Boniface Wambura
    REFA Hashim Abdallah wa Dar es Salaam, ndiye atakayechezesha mechi ya kesho ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Yanga na SC na Azam FC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Hashim atasaidiwa na Hamisi Chang’walu wa Dar es Salaam pia na John Kanyenye kutoka Mbeya, wakati mezani atakuwepo Oden Mbaga.
    Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea kesho  kwa mechi tatu, lakini macho na masikio ya washabiki wa mpira wa miguu yatakuwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Uwanja huo wa kisasa utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Yanga na makamu bingwa Azam. Ingawa Azam imecheza mechi moja zaidi, lakini timu hizo zinatofautishwa kwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa kwenye msimamo wa ligi huku kila moja ikiwa na pointi 36.
    Pia vinara wa ufungaji kwenye ligi kwa sasa wanatoka katika timu hizo mbili. Kipre Tchetche aliyepachika mabao tisa hadi sasa ndiye anayeongoza akifuatiwa na Didier Kavumbagu wa Yanga mwenye mabao manane.
    Iwapo timu yoyote itafanikiwa kuondoka na pointi tatu katika mechi hiyo itakuwa katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa.
    Hadi sasa, Yanga inaongoa ligi hiyo kwa pointi zake 36 sawa na Azam, lakini ina mchezo mmoja mkononi na wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
    Mechi nyingine za kesho ni Mgambo Shooting dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wakati Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa Polisi Dodoma kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
    Jumapili (Februari 24 mwaka huu), Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utakuwa katika hekaheka nyingine kwa Simba chini ya Mfaransa Patrick Liewig kuikabili Mtibwa Sugar inayonolewa na Nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Mecky Maxime.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: HASHIM KUCHEZESHA YANGA NA AZAM KESHO, KIBENDERA CHANG'WALU NA KANYEYE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top