• HABARI MPYA

  Monday, February 18, 2013

  MUSSA MUDDE AFIWA NA MWANAWE

  Mussa Mudde, pole sana kwa msiba kwa kipenzi chako

  KIUNGO Mganda wa Simba SC, Mussa Mudde amefiwa na mwanawe, aliyefariki dunia leo kwa ajali ya gari mjini Kampala, Uganda. 
  Mudde anatarajiwa kuondoka leo kwenda kwao, Uganda kwa shughuli za mazishi na uwezekano wa kushiriki mchezo wa marudiano dhidi Recreativo de Libolo ya Angola sasa ni mdogo.
  Kiungo aliyecheza kwa dakika 53 mechi ya jana dhidi ya Libolo, Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya kumpisha Amir Maftah, dhahiri ataiachia Simba SC pengo asiposhiriki mechi ya marudiano. Pole Mudde, Mungu aiweke pema peponi roho ya mwanao. Amin.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MUSSA MUDDE AFIWA NA MWANAWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top