• HABARI MPYA

    Thursday, February 28, 2013

    MPINGA BODA BODA CUP YAANZA LEO

    Kamanda Mpinga akionyesha jezi za Mpinga Cup

    Na Princess Asia
    KIONGOZI Mkuu wa maandalizi ya Mashindano ya Mpinga Cup, ametangaza zawadi mbalimbali zitakazotolewa kwa timu zitakazoshiriki katika michuano hiyo inayoshirikisha waendesha pikipiki, maarufu kama Boda Boda wa Dar es Saalam, yanayoanza leo katika viwanja vya Polisi Oysterbay na yatadumu kwa wiki moja.
    Akitangaza zawadi hizo, ASP Emilian Kamwanda ambaye ni msaidizi Mwandamizi wa polisi na Kiongozi wa maandalizi ya michuano ya mpinga cup alisema” leo tunayo furaha kutangaza zawadi mbalimbali za washindi katika mashindano hayo ambayo yana lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha pikiki (bodaboda). Na zawadi hizi ziko kama ifuatavyo
    Mshindi wa kwanza atapata Kombe, Pesa taslimu shilingi million moja, jezi  set moja, kofia ngumu (helmet) 15 pamoja na mpira 1, mshindi wa pili atapata pesa taslimu shilingi laki tano, jezi seti moja , kofia ngumu (helmet) 15 pamoja na mpira 1 na mshindi wa tatu atapata  pesa taslimu shilingi laki tatu, , kofia ngumu (helmet) 15 pamoja na mpira 1,
    Aidha zawadi zitatolewa kwa Mchezaji bora na Goalkeeper bora ambapo  kila mmoja atapata  pesa taslimu shilingi laki moja,  vocha za kufanya manunuzi Mr Price zenye thamani ya Laki moja na kofia ngumu (helmet) 1
    Timu tano zitakazoshindwa pia hazitaondoka hivihivi , zitazawadiwa kila moja mipra na kofia ngumu Helmet
    Mashindano ya Mpinga Cup yameandaliwa na Jeshi la polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani na kudhaminiwa na Airtel, Rotary club, Mr.Price, Home Shopping Center  pamoja na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ili kutoa elimu kwa waendesha pikipiki juu ya sheria mbalimbali za usalama , kuimarisha uelewa wao wa matumizi ya barabara kwa lengo la kuendelea kudhibiti  ajali za barabarani pamoja na elimu ya Polisi jamii.
    Mashindano haya yanatarajiwa kutimua mbio kuanzia tarehe leo katika viwanja vya Polisi Oysterbey   kwa kushirikisha timu 8 za waendesha pikipiki. Mpinga Cup itaendelea katika mikoa ya Kipolisi ya Ilala na Temeke na hatimaye kutafuta mshindi wa mkoa wa Dsm.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MPINGA BODA BODA CUP YAANZA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top