• HABARI MPYA

  Sunday, May 05, 2019

  MAN UNITED NJE LIGI YA MABINGWA BAADA YA SARE NA HUDDERSFIELD

  Kiungo Mfaransa wa Manchester United, Paul Pogba akiruka juu kupiga mpira dhidi ya beki Mjerumani wa Huddersfield, Erik Durm katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa John Smith leo timu hizo zikitoka sare ya 1-1. Man United ilitangulia kwa bao la Scott McTominay dakika ya nane kabla ya Isaac Mbenza kuisawazishia Huddersfield dakika ya 60.
  Kwa sare hiyo, Manchester United inafikisha pointi 66 baada ya kucheza mechi 37, ikibaki nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu England na kupoteza kabisa matumaini ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao, sasa ikipigania tiketi ya Europa League 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED NJE LIGI YA MABINGWA BAADA YA SARE NA HUDDERSFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top