• HABARI MPYA

  Thursday, January 03, 2019

  LUKAKU AGUSA MPIRA WA KWANZA NA KUFUNGA MAN U YASHINDA 2-0

  Victor Lindelof, Ander Herrera, Alexis Sanchez na Marcus Rashford wakimpongeza Romelu Lukaku (kulia) baada ya kuifungia Manchester United bao la kwanza dakika ya 64 akigusa mpira kwa mara ya kwanza, dakika moja tu baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Anthony Martial katika ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Newcastle United Uwanja wa St. James' Park. Bao la pili la Man United limefungwa na Rashford dakika ya 80 akimalizia pasi ya Alexis Sanchez na kwa ushindi huo wa nne mfululizo chini ya kocha mpya, wa muda, Ole Gunnar Solskjaer Mashetani Wekundu wanafikisha pointi 38 baada ya kucheza mechi 21, ingawa wanabaki nafasi ya sita nyuma ya Arsenal yenye pointi 41 za mechi 21 pia 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LUKAKU AGUSA MPIRA WA KWANZA NA KUFUNGA MAN U YASHINDA 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top