Na Hemed Kivuyo, DAR ES SALAAM
WAANDISHI wa Habari hasa wale wa Michezo baadhi yao huwa wananiudhi sana. Wamekuwa kama `Mbwa` anayekufukuzwa lakini baada ya muda anarudi kwakuwa kasikia harufu ya Nyama mahali pale.
Pamoja na waandishi kujipuuza wenyewe lakini baadhi ya wamiliki ama wahariri wa Vyombo hivyo walishaanzisha `mwendo` kuwapuuza waandishi wao kiasi cha waandishi kujizoelea na kushika kasi ya kujipuuza .
Ukichunguza utabaini kuwa baadhi ya wanaoitwa wahariri hawana sifa hizo ingawa uhariri hausomewi,lakini baadhi yao wana upeo `mbilikimo` kiasi cha kukera.
Wahariri hao wanalipwa kiasi kikubwa cha Fedha huku waandishi wanaomletea habari hizo hawalipwi kabisa au wakiliwa basi ni kiasi kidogo sana.
Waandishi wa Habari wakisikiliza kutoka kwa Waandaji wa mashindano ya gofu (Junior Championship) ndani ya ukumbi wa Gymkhana Club Alhamisi ya OKtoba 16 mwaka 2014. Lakini Waandishi hao walifukuzwa 'kama mbwa' wiki hii walipokwenda kwenye mazoezi ya timu ya taifa ya soka, Taifa Stars.
Unakuta Habari inayoletwa na Mwandishi inapachikwa hivyo hivyo bila kuhaririwa na wakati mwingine unakuta kile kilichoandikwa na Mwandishi Mhariri wake hakielewi hata kidogo,anakipachika vilevile .
Baadhi ya magazeti hasa upande wa Michezo `yanakera` Habari za Hovyo hovyo zilizoandikwa hovyohovyo .
Hivi karibuni Taifa stars ilikuwa ikifanya mazoezi katika viwanja vya Gymkhana lakini waandishi wa habari za Michezo walipofika katika viwanja hivyo hawakuruhusiwa kupiga picha wala kuingia ndani ya uzio wa viwanja hivyo.
Siulaumu uongozi wa TFF kwakuwa siyo wao waliyokataza waandishi wa Habari kufika mazoezini hapo.
Uongozi wa uwanja huo waliwakataza waandishi wa Habari kuingia humo Ndani na hawakuanza jana wala juzi.
Waandishi wetu wanaripoti kuwa wamezuiwa alaf mhariri anaandika naye anaipachika ili siku ipite .
Nini kinafuata? Baada ya kuzuiwa kuchukua na kutoa habari na baada ya kuandika Habari hiyo nini kinafuata?
Kinachoniudhi na kunitapisha ni pale uongozi wa uwanja huo unapokuwa na shughuli zao huwaita waandishi haohao na waandishi hao hukimbia haraka katika Habari hiyo.
Uongozi wa uwanja huo unapoandaa michezi ya TENIS huwaita waandishi wa Habari na kuwachekea `jino la pembe`.
Sijui ni dhiki sijui ni kiherehere tulichonacho!! Ni kwanini waandishi waandishi wa wa Habari za Michezo tuelendelee kuwanyenyekea viongozi wa uwanja huo wa Gymkhana? Ni kwani wanapoandaa mashindano yao wanatuita na kwenda?
Hebu tujitofautishe na na `Mbwa` anayepigwa na kukimbia lakini badae akiitwa anakuja! Tusiende tena katika viwanja hivyo. Acheni kulialia kwani Nyie mmejipangaje?
(Mwandishi wa makala haya ni mtangazaji wa Redio One na ITV, ambaye anapatikana kwa namba +255 655 250157 na +255 752 250157)

.png)
0 comments:
Post a Comment