KLABU ya Juventus imekamilisha usajili wa mshambuliaji Murgentina, Paulo Dybala kutoka Palermo kwa dau la Pauni Milioni 24.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alikuwa anahusishwa na kuhamia Chelsea, Manchester United na Arsenal baada ya kuwa msimu mzuri Italia, ambako amefunga mabao 13 katika mechi 35 za Ligi.
Lakini amechagua kubaki Italia na amesaini Mkataba wa miaka mitano na 'KIbibi Kizee' cha Turin, kwa sababu walionyesha dhamira haswa ya kumsajili na kuamua kuipotezea Ligi Kuu ya England.
Juventus imekamilisha usajili wa mshambuliaji Muargentina, Paulo Dybala kutoka Palermo kwa dau la Pauni Milioni 24
Dybala alizivutia klabu za Ligi Kuu ya England na zote Manchester United, Chelsea na Arsenal zilikuwa zinamtaka
Taarifa katika tovuti ya klabu hiyo imesema: "Juventus Football Club inaweza kutangaza kufikia makubaliano na Palermo juu ya huduma za Paulo Dybala, ambaye amesaini Mkataba wa miaka mitano.
"Ada ya Euro Milioni 32,itakayolipwa kwa zaidi ya minne, imekubaliwa, pamoja na ziada ya Euro Milioni 8 ambayo itategemea na kiwango cha mchezaji imekubaliwa pia,".
Akizungumza baada ya uhamisho huo, Dybala alisema kwamba: "Juventus ni klabu ambayo ilikuwa inanihitaji mimi zaidi. "Walifanya jitihada za dhati kunisajili na ndiyo maana nimefanya uamuzi,".


.png)
0 comments:
Post a Comment