KOCHA Mkuu wa Yanga SC, Hans van der Pluijm amesema kwamba anakwenda mapumziko nchini Ghana anakoishi, lakini pia atatumia fursa hiyo kutafuta wachezaji wa kuongeza nguvu katika kikosi chzke.
Pluijm aliyeondoka jana jioni Dar es Salaam, amesema kwamba, kwanza atatafuta mchezaji atakayeziba pengo la Mrisho Ngassa (pichani kulia) aliyehamia Free State Stars ya Afrika Kusini, baada ya hapo mengine yatafuata.
Kocha huyo wa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, amesema kwamba ameelekeza nguvu zake nchini Ghana katika kumtafuta mrithi wa Ngassa aliyekuwa tegemeo la Yanga.
![]() |
| Hans van der Pluijm (kushoto) akiwa na Msaidizi wake, Charles Boniface Mkwasa |
“Natafuta mchezaji atakayeziba nafasi ya Ngassa, ambaye atakuwa na uwezo mkubwa wa kuisaidia timu kama ilivyokuwa kwa Ngassa,”amesema Pluijm.
Kwa ujumla kocha huyo Mholanzi, amesema katika usajili wake wa kikosi cha msimu ujao atahitaji wachezaji wenye uwezo wa kumudu mikiki ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
“Nataka kuwa na timu ambayo hata tukipangiwa timu yoyote katika Ligi ya Mabingwa tunakuwa hatuna wasiwasi. Nataka aina ya wachezaji ambao nikiwa nao kwenye timu watanisaidia,”amesema Pluijm.




.png)
0 comments:
Post a Comment