• HABARI MPYA

    Friday, May 15, 2015

    APR WAWEKA REKODI RWANDA, WATWAA TAJI LA 15 NFL

    Jean Baptiste Mugiraneza wa APR
    APR imetwaa ubingwa wa Ligi ya Taifa (NFL) Rwanda ikiwa imebakiza mechi mbili mkononi, baada ya kufikisha pointi 51, tano zaidi ya AS Kigali walio nafasi ya pili, ambao wana mechi moja.
    Timu hiyo ya jeshi imetwaa taji lao la rekodi la 15 katika miaka 22 tangu waanze kucheza Ligi ya Rwanda mwaka 1993 kufuatia sare ya 1-1 na AS Kigali viwanja vya FERWAFA jana jioni.
    Nahodha wa APR, Ismael Nshutiyamagara ameelezea furaha yake juu ya mafanikio hayom akisema; “Tulistahili taji la ubingwa kwa sababu tulijituma sana msimu huu. Haya ni malipo ya kazi ngumu.”
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: APR WAWEKA REKODI RWANDA, WATWAA TAJI LA 15 NFL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top