• HABARI MPYA

    Saturday, May 16, 2015

    PIET DE MOL AJA KURITHI MIKOBA YA ‘CHA MARINGO’ KOPUNOVIC SIMBA SC

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mbelgiji, Piet de Mol (pichani juu) atatua Dar es Salaam Mei 21, mwaka huu kwa ajili ya mazungumzo ya kuifundisha Simba SC.
    Lakini kutua kwa Mbelgiji huyo kutategemea na msimamo wa mwisho wa Simba SC juu ya kocha wake wa sasa, Goran Kopunovic raia wa Serbia.
    Kopunovic aliondoka mapema wiki hii kurejea kwao kwa mapumziko, lakini akiwa hajasaini Mkataba mpya baada ya huu wa sasa wa miezi sita kukamilika.
    Tatizo ni kwamba, Goran ametaka mshahara mkubwa dola za Kimarekani 9,000 (Sh. Milioni 18) na ada ya kusaini Mkataba dola 50,000 (Sh. Milioni 100), ambazo Simba imemuambia haina uwezo huo.
    Kopunovic akaondoka kwenda mapumzikoni, akisema kwamba angetoa jibu jana Ijumaa kama amekubali ofa ya uongozi au la. Lakini hadi jana jioni hakukuwa na taarifa zozote kuhusu Mserbia huyo anayeishi Bulgaria kwa sasa. 
    Maana yake kuna uwezekano, de Mol mwenye umri wa miaka 60 na uzoefu mkubwa wa kufundisha soka Afrika, Asia na Ulaya akarithi mikoba ya Kopunovic.
    Piet Demol alipookuwa Ghana mwaka jana

    Mwaka jana, Piet de Mol alikuwa nchini Ghana akifanya kazi kama Mkurugenzi wa Ufundi wa akademi mjini Kumasi
    Mbali na Ghana ambako alifanya kazi na Asante Kotoko, De Mol amefundisha timu pia kwao Ubelgiji, Dubai, Qatar na China. Alikuwa kocha Msaidizi wa AA Gent kuanzia mwaka 1997 hadi 2001.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PIET DE MOL AJA KURITHI MIKOBA YA ‘CHA MARINGO’ KOPUNOVIC SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top