• HABARI MPYA

    Saturday, May 16, 2015

    AZAM, SIMBA, YANGA ZAGOMBEA SAINI YA DEUS KASEKE, MWENYEWE ASEMA; “MIMI HELA TU”

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    WINGA mwenye kasi na krosi maridadi, Deus Kaseke (pichani kushoto) amesema kwamba amebakiza siku 28 tu katika Mkataba wake na Mbeya City, wakati huo huo, vigogo, Azam, Simba na Yanga wote wanamtaka.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana, Kaseke kwamba bado hajaamua asaini wapi, kwani anasikilizia timu itakayotoa dau kubwa ndiyo aipe saini yake.
    “Mimi ni maslahi tu, nawasikiliza sikiliza wote, yule ambaye mwisho wa siku ataniita mezani ndiye tutamalizana. Mimi kama mchezaji naangalia maslahi, kwa sababu mpira ndiyo kazi yangu,”amesema.
    Kaseke amekuwa akitajwa Yanga SC kama mchezaji anayefaa kwenda kuziba pengo la Mrisho Ngassa aliyehamia Free State Stars ya Afrika Kusini.
    Wakati huo huo, kuna habari Azam FC na Simba SC nao wanaisaka saini ya mchezaji huyo tegemeo a Mbeya City. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM, SIMBA, YANGA ZAGOMBEA SAINI YA DEUS KASEKE, MWENYEWE ASEMA; “MIMI HELA TU” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top