• HABARI MPYA

    Saturday, May 16, 2015

    COSAFA 2015; ACHA MOTO UWAKE RUSTENBURG, ZIMBABWE WAANZA ‘KUKINUKISHA’ MORULENG

    Na Mahmoud Zubeiry, RUSTENBURG
    MICHUANO ya Kombe la Mataifa ya kusini mwa Afrika COSAFA, mwaka 2015 inaanza kesho mjini hapa, Rustenburg, jimbo la Kaskazini Magharibi, Afrika Kusini.
    Michuano hiyo ya 15 itashirikisha timu 14, zikiwemo mbili, Tanzania na Ghana wageni waalikwa. Timu nyingine ni Mauritius, Shelisheli, 
    Swaziland, Madagascar, Zimbabwe, Namibia,
    Lesotho , Botswana, Malawi, Msumbiji, Zambia na wenyeji Afrika Kusini.
    Kundi A lina timu za Namibia, Mauritius, Shelisheli na Zimbabwe, wakati Kundi B lina timu za Lesotho, Madagascar, Swaziland na Tanzania. 
    Tanzania imepangwa kundi mchekea B, pamoja na Lesotho, Madagascar na Swaziland
    Kundi A

    PosTeamPldWDLGFGAGDPts
    1 Namibia00000000
    2 Mauritius00000000
    3 Shelisheli00000000
    4 Zimbabwe00000000
    Kundi B
    PosTeamPldWDLGFGAGDPts
    1 Lesotho00000000
    2 Madagascar00000000
    3 Swaziland00000000
    4 Tanzania00000000
    Mshindi wa kila kundi ataungana na wenyeji Afrika Kusini, Msumbiji, Zambia, Ghana, Botswana na Malawi kucheza Robo Fainali.
    Kutakuwa na Nusu Fainali za aina mbili, kwanza za timu zilizofungwa katika Robo Fainali (Plate Semi Finas) na zilizoshinda (Semis Finals).
    Vibonde wataendelea kupepetana hadi fainali yao ambayo itapigwa Mei 29, wakati fainali ya wakali itakuwa Mei 30.
    Ghana ndiyo timu inayoongoza kwa ubora wa soka katika nchi zinazoshiriki COSAFA mwaka huu

    VIWANGO VYA UBORA;
    Shelisheli ndiyo nchi duni zaidi kisoka kati ya timu zinazoshiriki COSAFA ya mwaka huu, ikiwa inashika nafasi ya 187, Mauritius 185, Swaziland 165, Madagascar 148, Zimbabwe 119, Namibia 111, Lesotho 125, Tanzania 107, Botswana 105, 
    Malawi 93, Msumbiji 90, Zambia 60, Afrika Kusini 56, wakati Ghana ndiyo ‘baba lao’ nafasi ya 25. Angola na Comoro zimejitoa.

    RATIBA KAMILI COSAFA 2015
    Mei 17, 2015
    Namibia v Shelisheli (Saa 9:00 Alasiri, Uwanja wa Moruleng) 
    Zimbabwe v Mauritius (Saa 11:30 jioni Uwanja wa Moruleng) 
    Mei 18, 2015
    Lesotho v  Madagascar (Saa 11:30 jioni Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace)
    Tanzania v Swaziland (Saa 1:30 usiku Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace)
    Mei 19, 2015
    Shelisheli v Zimbabwe (Saa 11:00 jioni Uwanja wa Moruleng) 
    Namibia v Mauritius (Saa 1:30 usiku Uwanja wa Moruleng) 
    Mei 20, 2015
    Madagascar v Tanzania (Saa 11:00 jioni Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace)
    Lesotho v Swaziland (Saa 1:30, usiku Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace)
    Mei 21, 2015
    Namibia v  Zimbabwe (Saa 11:00 jioni Uwanja wa Moruleng) 
    Shelisheli v  Mauritius (Saa 11:00 jioni Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace)
    Mei 22, 2015
    Lesotho  v Tanzania (Saa 11:00 jioni Uwanja wa Moruleng)
    Madagascar v Swaziland (Saa 11:00 jioni Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace) 
    Wenyeji Afrika Kusini wanapewa nafasi kubwa ya kubakiza taji nyumbani

    ROBO FAINALI
    Mei 24, 2015
    Ghana v Mshindi Kundi B (Saa 9:00 Alasiri Uwanja wa Moruleng)
    Msumbiji v Malawi (Saa 11:30 Uwanja wa Moruleng) 
    Mei 25, 2015
    Zambia v Mshindi Kundi A (Saa 11:30 Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace)
    Afrika Kusini v Botswana (Saa 1:30 usiku Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace)
    NUSU FAINALI ZA VIBONDE
    Mei 27, 2015
    Saa 11:00 jioni Uwanja wa Moruleng
    Saa 1:30 usiku Uwanja wa Moruleng
    FAINALI YA VIBONDE
    Mei 29, 2015
    Saa 11:00 jioni Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace
    NUSU FAINALI
    Mei 28, 2015
    Saa 11:00 jioni Uwanja wa Moruleng 
    Saa 1:30 usiku Uwanja wa Moruleng 
    MSHINDI WA TATU
    Mei 30, 2015
    Saa 9:00 Alasiri Uwanja wa Moruleng 
    FAINALI
    Saa 11:30 jioni Uwanja wa Moruleng 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: COSAFA 2015; ACHA MOTO UWAKE RUSTENBURG, ZIMBABWE WAANZA ‘KUKINUKISHA’ MORULENG Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top