• HABARI MPYA

    Friday, April 03, 2015

    YANGA SC WAGANDISHWA ‘AIRPORT DAR’ TANGU ASUBUHI HADI SAA SABA

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    WACHEZAJI wa Yanga SC ndio wanapanda ndege saa saba hii mchana, tayari kwa safari ya Bulawayo, Zimbabwe baada ya kugandishwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) tangu saa 4:00 asubuhi kwa sababu uongozi wa klabu hiyo ulikuwa haujalipia ndege.
    Yanga SC imekodi ndege ya Serikali kwenda Bulawayo, Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, FC Platinum.
    Hata hivyo, inadaiwa uongozi wa ndege uligoma kuwapakia wachezaji hao hadi malipo yafanyike- lakini inaelezwa hivi sasa suala hilo limekwishatatuliwa na wachezaji ndiyo wanapanda ndege tayari kuondoka.

    Wachezaji wa Yanga walipumzika kwenye makochi ya JNIA tangu saa nne asubuhi na mchana huu wa saa  saba ndiyo wanaondoka kuelekea Zimbabwe

    Kikosi cha wachezaji 18 wa Yanga SC kinakwenda Bulawayo, Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa marudiano hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho Afrika.
    Platinum wanatakiwa kushinda mabao 4-0 Uwanja wa Mandava kesho ili kwenda 16 Bora ya Kombe la Shirikisho, baada ya awali timu hiyo yenye maskani yake Zvishavane kufungwa mabao 5-1 Dar es Salaam.
    Wachezaji wanaoondoka ni makipa Deo Munishi ‘Dida’ na Ally Mustafa ‘Barthez’, mabeki Juma Abdul, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Pato Ngonyani, Rajab Zahir, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kevin Yondan.
    Viungo ni Salum Telela, Said Juma, Nizar Khalfan, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Mrisho Ngassa na washambuliaji Danny Mrwanda, Amisi Tambwe na Hussein Javu.
    Benchi la Ufundi litaongozwa na Kocha Mkuu, Mholanzi, Hans van der Pluijm, Msaidizi wake Charles Boniface Mkwasa, kocha wa makipa Juma Pondamali, Meneja Hafidh Saleh, Daktari Sufiani Juma, mtunza vifaa, Mahmoud Omar ‘Mpogolo’ na Mchua misuli Jacob Onyango.
    Timu hiyo inatarajiwa kuondoka kuanzia Saa 4:00 asubuhi kwa ndege maalum ya kukodi ya serikali na itafikia katika hoteli ya Rainbow na jioni itakwenda kufanya mazoezi ya kuuzoea Uwanja wa Mandava, umbali wa kilomita 200.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC WAGANDISHWA ‘AIRPORT DAR’ TANGU ASUBUHI HADI SAA SABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top