• HABARI MPYA

    Thursday, April 30, 2015

    SIMBA WATAKIWA KUMLIPA CHANONGO MILIONI 11. 4

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    KLABU ya Simba SC inatakiwa kumlipa mchezaji Haroun Chanongo (pichani kulia) Sh. 11, 400,000,  kufikia Aprili 30, 2015 vinginevyo Sekretarieti ya TFF itaanza kukata mapato ya Simba ili kumlipa mchezaji huyo. 
    Iwapo Simba itakuwa na vielelezo vingine katika kikao kinachofuata cha Kamati kitakachofanyika Mei 3, 2015 itafanywa hesabu na Simba kurejeshewa fedha itakayokuwa imezidi.
    Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF imeagiza kwa klabu ya Simba na klabu nyingine zote kuwa kwa wachezaji wa mkopo, maslahi yao (mishahara na posho) yote yailipwe na klabu husika kwa klabu ambayo mchezaji anakwenda kwa mkopo ili malipo yake yawe yanafanyika kutoka kwenye klabu moja badala ya kufuatilia malipo yake katika klabu mbili tofauti, hali hii inaweza msabababishia usumbufu mchezaji aliye kwenye mkopo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA WATAKIWA KUMLIPA CHANONGO MILIONI 11. 4 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top