• HABARI MPYA

    Wednesday, April 29, 2015

    KILIMANJARO PREMIUM LAGER NA BASATA WATANGAZA WATEULE WA VINYANG’ANYIRO VYA TUZO ZA MUZIKI TANZANIA (KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS).

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    BARAZA la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa kushirikiana na Kilimanjaro Premium Lager leo wametangaza rasmi wateule (Nominees) wa vinyang’anyiro 32 vya tuzo za Muziki Tanzania (Kilimanjaro Tanzania Music Awards).
    Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, meneja wa bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli alisema “Academy ilikaa mwisho wa wiki iliopita na kufanya kazi ngumu na nzito ya kupitia mapendekezo ya umma na hatimae kuteua kwa njia ya kupiga kura, wasanii wa muziki, watunzi wa mashairi ya muziki na watengeneza kazi za muziki (Producers) waliofanya kazi nzuri na zilizopendwa na kukubalika zaidi na wengi kwa mwaka 2013/2014”. 
    Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa kutaja orodha ya wanamuziki wanaowania tuzo. Kulia ni Ofisa wa BASATA, Kurwijira Maregesi na kushoto Pavel Gabriel wa Auditax International, waratibu wa zoezi la kura 

    Pamela aliendelea kueleza ni jinsi gani zoezi la kupata wateule hawa lilivodumu kwa muda wa zaidi ya saa 18 kudhihirisha umahiri na kujituma kwa kundi la Academy kuhakikisha KTMA inapata wateule sahihi. ‘Wana Academy wanastahili pongezi ya kipekee na Kilimanjaro inapenda kutambua mchango wao katika mchakato huu na kwamba tutaendelea kushirikiana nao kwa karibu katika mpango wa kuendelea kuziboresha tuzo hizi’, alisema Pamela.
    Kwa upande wa BASATA, walipenda uma utambue mabadiliko madogo yalioyalzimika kufanyika kwenye mchakato wa Academy katika maslahi ya kuenzi na kutangaza kazi za kundi maalum la wana muziki. Kuna vipengele vvitatu vilitengenezwa kwa malengo mahsusi navyo ni; vya bendi, muziki wa asili ya ki Tanzania pamoja na Reggae. Nia ya kuanzishwa kwa vipengele hivi ilikua ni kukuza muziki husika ambao haupati muda mwingi kwenye vyombo vya habari ili kusikika kama ilivo miziki pendwa. Mwaka huu BASATA iliamua kuweka msisitizo na mkazo kwenye hilo na kwamba kipengele cha bendi kinatizama bendi zinazopiga muziki wa dansi tu kama itakavoonekana kwa wateule wake. Kipengele cha muziki wenye vionjo vya asili utatizama muziki halisi wa kitamaduni wa Tanzania na si vionjo kama ilivoeleweka halikadhalika reggae kimetoa nafasi kwa waimbaji wa miondoko halisi wa reggae na si waimbaji wa miondoko mengine (muziki pendwa).
    ‘Nia ya BASATA ni kuendeleza na kukuza muziki wa Tanzania ikiwa ni pamoja na bendi za dansi ambazo hazipati airplay ya kutosha kadhalika kwa miziki ya asili na reggae’. Alisema Bw. Maregesi ambae ni Mratibu wa tuzo za muziki kutoka BASATA.
    Mchakato wa Academy ulisimamiwa na wasimamizi wa mahesabu na utawala AUDITAX International ili kuhakikisha zoezi linafanywa kwa uhuru na haki muda wote. Pavel Gabriel wa Auditax aliwathibitishia wana habari kwamba kwa mujibu wa utaratibu Academy ilipitia mapendekezo na kupiga kura kwa usiri na matokeo ni halali.
    Tanzania itapewa nafasi kuanza kupiga kura kwa kutumia njia zile zile ili kuchagua mshindi kwa kila kipengele. Kura zitaanza kupigwa tarehe 4 Mei 2015 had tarehe 5 Juni 2015. Njia za kupiga kura ni kama zifwatazo:
    1. Whatsapp – 0686 528 813.
    2. SMS – 15415.
    3. Mtandao – www.ktma.co.tz
    Kwa taarifa zaidi:
    Pamela Kikuli, Brand Manager, Mob: +255 767 266 415, Email: pamela.kikuli@tz.sabmiller.com, www.ktma.co.tz Kurwijira Maregesi – Mratibu wa tuzo za muziki Tanzania, BASATA +255 784 861 529 Email: kurwij@yahoo.com
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KILIMANJARO PREMIUM LAGER NA BASATA WATANGAZA WATEULE WA VINYANG’ANYIRO VYA TUZO ZA MUZIKI TANZANIA (KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS). Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top