Na Vincent Malouda, NAIROBI
AZAM TV itawapa watazamaji wake burudani kamili kwa kuwapeperushia mechi mbili za ligi kuu ya Shirikisho la Soka Kenya, FKF, wikiendi ijayo.
Mechi ya kwanza itakuwa Jumamosi 4 Aprili uwanjani Kasarani baina ya FC Talanta dhidi ya Zoo Kericho tangia saa tisa alasiri huku ya pili ikitangazwa siku ya jumapili 5 Aprili Posta Rangers ikidanadana na Agrochemicals uwanjani Kasarani mida ya saa tisa alasiri.
Katika ratiba ya mechi zingine kwenye ligi hiyo, Moyas itachuana na Ligi Ndogo - Kasarani huku Kakamega Homeboyz wakimenyana na Kariobangi Sharks ugani Bukhungu, Nzoia United na Shabana uwanja wa Kandui na Oserian wapambane na St. Joseph katika uchanjaa wa Oserian siku ya jumamosi.
Jumapili, Nakumatt itapenua uwanja wa Kasarani baina ya Modern Coast saa saba kisha Rangers na Agro kwenye Azam TV saa tisa. Kwingineko, West Kenya watagaragazana na Finlays kule Bukhungu, mechi zote ziking'oa nanga saa tisa alasiri.
Kwenye ligi ya Kampuni inayosimamia ligi kuu, KPL, Chemelil Sugar watawakaribisha Tusker FC ugani Chemelil hapo kesho Jumamosi katika mechi pekee ya siku hiyo.
Nayo jumapili, AFC Leopards yake Zdravko Logarusic ikabiliane na Thika United ugani Mumias, Mathare United dhidi ya City Stars - Machakos, Western Stima na Sofapaka - Kisumu, Nakuru AllStars na SoNy Sugar Afraha nayo Ushuru FC anapochezea Mzalendo David Naftali Tevelu iwatembelee Muhoroni Youth kwao Muhoroni.
Mechi zote zitaanza saa tisa alasiri. Kumbuka timu sita zitapandishwa ngazi kwenye ligi ya FKF huku nne zikitemwa ligi ya KPL ili kutengeza timu 18 zitakazoshiriki ligi kuu msimu wa 2016 kuendelea kama walivyokubaliana FKF na KPL baada ya washikadau wa FIFA wakiongozwa na rais wa Shirikisho la Soka la Ghana, Kwesi Nyantakye kuingilia kati kwenye mojawapo wa suluhisho kwa mgogoro uliyokuwepo hapo awali kuhusu nani atakayesimamia ligi kuu na idadi ya timu zitazoshiriki.

.png)
0 comments:
Post a Comment