• HABARI MPYA

    Thursday, April 30, 2015

    YANGA SC ‘WACHOMESHWA’ SAA MBILI UWANJA NDEGE TUNIS, WAPEWA BASI KUSAFIRI KILIMOTA 140 KUWAFUATA ETOILE ‘KIJIJINI KWAO’

    Na Prince Akbar, TUNIS
    MSAFARA wa Yanga SC imetua salama mjini Tunis na baada ya kugandishwa kwa saa zaidi ya mbili Uwanja wa Tunis, imeanza safari ya basi kuelekea mji mdogo wa Sousse kwa wenyeji wao, Etoile du Sahel umbali wa kilomita 140.
    Yanga SC iliondoka usiku wa jana kwenda Tunisia kwa ajili ya mchezo wa marudaino hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika mwishoni mwa wiki.
    Wachezaji walio safarini na Yanga SC ni makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’, mabeki Pato Ngonyani, Oscar Joshua, Edward Charles, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ’Juma Abdul, Rajab Zahir, Mbuyu Twite na Kevin Yondan.
    Wachezaji wa Yanga SC wakiwa Uwanja wa Ndege wa Tunis, ambako waligandishwa saa zaidi ya mbili kusubiri basi la kuwapeleka mji mdogo wa Sousse 


    Viungo ni Nizar Khalfan, Andrey Coutinho, Salum Telela na Said Juma ‘Makapu’, wakati washambuliaji ni Hussein Javu, Amissi Tambwe, Kpah Sherman, Mrisho Ngasa, Jerry Tegete na Simon Msuva. 
    Yanga SC inahitaji ushindi wa ugenini au sare kuanzia mabao 2-2 kufuatia kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Etoile katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam wiki iliyopita.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC ‘WACHOMESHWA’ SAA MBILI UWANJA NDEGE TUNIS, WAPEWA BASI KUSAFIRI KILIMOTA 140 KUWAFUATA ETOILE ‘KIJIJINI KWAO’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top