• HABARI MPYA

    Tuesday, April 28, 2015

    TFF YAITIWA FEDHA BANK

    Na Hemed Kivuyo, DAR ES SALAAM
    MKURUGENZI Mtendaji wa Covenant Bank Sabetha Mwambenja, amewaita viongozi wa Soka Nchini TFF, kwenda kujadili namna ambavyo benki hiyo inaweza kuisaidia Timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars ambayo imefuzu kushiriki Michuano ya All African Games itakayo fanyika nchini Congo mwezi septemba.
    Hayo yametanabaishwa na Mkurugenzi huyo katika hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya Lucenti inayoshiriki michuano ya kanda ya nyanda za juu kusini yatakayo fanyika Sumbawanga baada ya kufudhu michezo ya ligi dalaja la tatu baada ya kuulizwa swali na waandishi waliotaka kujua ni namna gani benki hiyo inaweza kuisaidia timu hiyo ya Taifa inayosuasua katika maandalizi.

    Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, (Katikati) Mwenyekiti wa Klabu ya Lucenti, Yusuph Liambe, Mkurugenzi wa Bodi ya Benki hiyo Margreth Kyarwenda wakiwa wameshikilia vifaa vya michezo vilivyotolewa na Covenant Bank kwa timu hiyo itakayoshiriki michuano ya kanda ya nyanda za juu kusini itakayofanyika Sumbawanga Mkoani Rukwa.

    “Hatuna tatizo katika kuisaidia timu ya Taifa ya Wanawake tunaweza kuwasaidia kulingana na Mahitaji yao, ni vyema viongozi wa soka (TFF) waje tukae tujadiliane ni Namna gani tunaweza kuisaidia timu yetu ya taifa ili kuhakikisha inafanya vizuri katika michuano hiyo inayokuja na mingine yote” alisema Mkurugenzi huyo.
    Akikabidhi vifaa hivyo kwa timu hiyo, kukabidhi vifaa hivyo iliyofanyika kwenye makao mkuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi huyo, alisema wameamua kuvitoa ikiwa ni sehemu ya kutambua ushirikiano wao na wananchi wa mkoa wa Ruvuma hususani wilaya ya Namtumbo.
    “Tumekuwa tukishirikiana kwa masuala mengi ya kijamii na wanachi wa Namtumbo, tumesaidia kujenga madarasa katika shule za msingi na maabara kwa shule za sekondari wilayani humo kuwasadia ndugu zetu kukamilisha maagizo ya Rais yanayolenga kuinua masomo ya sayansi nchini,” alisema.
    “Kwa kutambua umuhimu wa michezo, tumeona ni vyema tuchangie pia maendeleo ya soka katika wilaya ya Namtumbo kwa kuipa vifaa vya michezo klabu ya Lusenti.”
    Baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo vya Michezo, Yusuph Liambe, mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Namtumbo, aliushukuru uongozi wa Benki ya Covenant kwa kutambua umuhimu wa sekta ya michezo nchini na kuwapa vifaa hivyo ambayo alisema anaamini vitaleta chachu ya timu ya Lusenti kufanya vyema katika mashindano ya soka ngazi ya kanda yatakayoanza Mei 2, mwaka huu.
    Katika mashindano hayo yanayotambuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), klabu ya Lusenti imepangwa Kanda ya Kusini pamoja na timu nyingine tisa kutoka mikoa ya Njombe, Mbeya na wenyeji wa kanda hiyo mkoa wa Rukwa.
    “Tunaamini vifaa hivi vitawapa nguvu wachezaji wetu kujituma na kufanya vyema katika michuano ya kanda, hivyo vipaji vyao kuonekana na kuchukuliwa na timu kubwa ambazo zitawapa ajira,” alisema Liambe ambaye pia ni mwenyekiti wa klabu ya soka ya Lusenti.
    Vifaa vya michezo vilivyotolewa jana na benki hiyo ni pamoja na jezi seti nne, viatu na mipira ya mazoezi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAITIWA FEDHA BANK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top