• HABARI MPYA

    Tuesday, April 28, 2015

    LIGI YA MABINGWA WA MIKOA SASA MEI 9

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    LIGI ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) sasa itaanza Jumamosi Mei 9, 2015 badala ya Jumamosi Mei 2, 2015 kama ilivyokua imetangazwa awali.
    Uamuzi huo umefanyika ili kutoa fursa kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kukamilisha maandalizi ya mwisho ikiwemo ukaguzi wa viwanja ambavyo vitatumika katika RCL na masuala mengine ya kumsingi.
    Tunaomba radhi kwa usumbufu ambao utakuwa umejitokeza kutokana na taarifa hii ya kusogeza mbele kuanza kwa ligi, lakni pia kuzitakia kila la kheri timu zinazoshiriki katika maandalizi yao. Ratiba ya mashindano itatolewa/kutumwa leo kama ilivyopangwa awali.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIGI YA MABINGWA WA MIKOA SASA MEI 9 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top