Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
KOCHA wa Azam FC George ‘Best’ Nsimbe amefurahia kurejea kwa kiungo wake hodari mkabaji, Kipre Michael Balou akisema kutaongeza nguvu katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Balou anatarajiwa kurejea uwanjani wiki ijayo, baada ya kukosekana kwa wiki tatu kutokana na maumivu ya msuli wa paja la kulia.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo, Nsimbe amesema katika harakati za ubingwa inapendeza kuwa na wachezaji wako wote unaowategemea, hivyo kurejea kwa Balou ni faraja kwake.
“Hiyo si kwa Azam FC, timu yoyote itapenda kuwa na wachezaji wake wote tegemeo wakati wa harakati kama hizi za ubingwa, hivyo nasi tunafurahi Balou amerudi,”amesema.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wanaendelea na mazoezi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kujiandaa na mechi dhidi ya Mbeya City Jumatano ijayo.
Azam FC wataikaribisha Mbeya City Aprili 8, Uwanja wa Azam Complex katika mfululizo wa Ligi Kuu, huo ukiwa mchezo wa marudiano baada ya awali timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake kushinda 1-0 Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Mbali na Balou, raia wa Ivory Coast aliyetua Chamazi miaka mitatu iliyopita, majeruhi wengine ambao bado wanajiuguza ni kiungo mshambuliaji Khamis Mcha ‘Vialli’ anayesumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu sawa na beki wa pembeni, Waziri Salum.

![]() |
| Kipre Balou kulia amerejea kikosini Azam FC baada ya wiki tatu za kuwa nje kwa maumivu ya msuli wa paja la kulia |
“Hiyo si kwa Azam FC, timu yoyote itapenda kuwa na wachezaji wake wote tegemeo wakati wa harakati kama hizi za ubingwa, hivyo nasi tunafurahi Balou amerudi,”amesema.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wanaendelea na mazoezi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kujiandaa na mechi dhidi ya Mbeya City Jumatano ijayo.
Azam FC wataikaribisha Mbeya City Aprili 8, Uwanja wa Azam Complex katika mfululizo wa Ligi Kuu, huo ukiwa mchezo wa marudiano baada ya awali timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake kushinda 1-0 Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Mbali na Balou, raia wa Ivory Coast aliyetua Chamazi miaka mitatu iliyopita, majeruhi wengine ambao bado wanajiuguza ni kiungo mshambuliaji Khamis Mcha ‘Vialli’ anayesumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu sawa na beki wa pembeni, Waziri Salum.

.png)
0 comments:
Post a Comment