Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI wa TP Mazembe, Thomas Ulimwengu (pichani kulia) amesema watapigana ‘kufa na kupona’ Jumapili kuhakikisha wanaitoa Mamelodi Sundowns katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Tout Puissant Mazembe inawakaribisha Mamelodi Sundowns FC Jumapili Uwanja wa TP Mazembe mjini Lubumbashi katika mchezo wa marudiano hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mazembe wenye mshambuliaji mwingine Mtanzania, Mbwana Samatta wanatakiwa kushinda 2-0 ili kusonga mbele, baada ya awali kufungwa 1-0 Afrika Kusini na Ulimwengu amesema; “Inawezekana”.
“Sisi kuwafunga 2-0, au 3-0 hata zaidi hapa kwetu inawezekana, lakini ni lazima tupigane sana uwanjani, kwa sababu hata wao watakuja kupambana kuulinda ushindi wao,”amesema Ulimwengu.
Uli amesema kikosi chao kipo vizuri kuelekea mchezo huo na jana walicheza mechi ya kujipima nguvu dhidi ya Lubumbash Sport wanayocheza nayo Ligi Kuu ya DRC wakashinda 5-2.
“Tunatoka kucheza mechi ya kirafiki, tumeshinda 5-2, mimi nimefunga moja na Mbwana (Samatta) moja. Ni sehemu ya maandalizi yetu ya mechi na Mamelodi,”amesema Ulimwengu.
Mwaka jana, Mazembe ilitolewa na ES Setif ya Algeria katika Nusu Fainali ya michuano hiyo kwa mabao ya ugenini, baada ya sare ya jumla ya 4-4 kufuatia kufungwa 2-1 Algeria na kushinda 3-2 nyumbani.
Setif ilikwenda na kuifunga pia AS Vita ya DRC kwa mabao ya ugeini baada ya sare ya 3-3 Kinshasa na 1-1 Setif hivyo kutwaa Kombe la Afrika.
MSHAMBULIAJI wa TP Mazembe, Thomas Ulimwengu (pichani kulia) amesema watapigana ‘kufa na kupona’ Jumapili kuhakikisha wanaitoa Mamelodi Sundowns katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Tout Puissant Mazembe inawakaribisha Mamelodi Sundowns FC Jumapili Uwanja wa TP Mazembe mjini Lubumbashi katika mchezo wa marudiano hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mazembe wenye mshambuliaji mwingine Mtanzania, Mbwana Samatta wanatakiwa kushinda 2-0 ili kusonga mbele, baada ya awali kufungwa 1-0 Afrika Kusini na Ulimwengu amesema; “Inawezekana”.
Uli amesema kikosi chao kipo vizuri kuelekea mchezo huo na jana walicheza mechi ya kujipima nguvu dhidi ya Lubumbash Sport wanayocheza nayo Ligi Kuu ya DRC wakashinda 5-2.
“Tunatoka kucheza mechi ya kirafiki, tumeshinda 5-2, mimi nimefunga moja na Mbwana (Samatta) moja. Ni sehemu ya maandalizi yetu ya mechi na Mamelodi,”amesema Ulimwengu.
Mwaka jana, Mazembe ilitolewa na ES Setif ya Algeria katika Nusu Fainali ya michuano hiyo kwa mabao ya ugenini, baada ya sare ya jumla ya 4-4 kufuatia kufungwa 2-1 Algeria na kushinda 3-2 nyumbani.
Setif ilikwenda na kuifunga pia AS Vita ya DRC kwa mabao ya ugeini baada ya sare ya 3-3 Kinshasa na 1-1 Setif hivyo kutwaa Kombe la Afrika.

.png)
0 comments:
Post a Comment