• HABARI MPYA

    Friday, April 03, 2015

    CHELSEA YAUNGANA NA MAN CITY, ARSENAL KUWANIA SAINI YA RAHEEM STERLING

    KLABU ya Chelsea imeungana na Arsenal na Manchester City katika vita ya kuwania saini ya kinda wa kimataifa wa England, Raheem Sterling.
    Chelsea imejiweka mkao wa kumchukua Sterling, licha ya kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers kusistiza kinda wake wa umri wa miaka 20 hataondoka kwenda popote mwishoni mwa msimu.
    Sterling aliwachanganya Liverpool mapema wiki hii baada ya kusema kwamba havutiwi fedha ili kusaini Mkataba mpya wa Pauni 100,000 kwa wiki, bali anataka kufurahia mataji. Mchezaji huyo pia, alishangazwa na habari za yeye kutaka kuhamia Arsenal. Imezua wasiwasi mkubwa kwamba, Sterling, ambaye amekulia London na kuibukia katika mfumo wa soka ya vijana wa QPR, anataka kurejea katika jiji hilo.  
    Sterling amesema havutiwi fedha kusaini Mkataba mpya qa Pauni 100,000 kwa wiki Liverpool
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHELSEA YAUNGANA NA MAN CITY, ARSENAL KUWANIA SAINI YA RAHEEM STERLING Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top