Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba ataachwa mchezaji mmoja wa kigeni mwishoni mwa msimu kati ya waliopo sasa ili kusajiliwa Mkenya Paul Kiongera.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana mjini Dar es Salaam, Hans Poppe alisema kwamba uamuzi wa nani aachwe utafanywa na kocha wao, Mserbia Goran Kopunovic.
Wachezaji wa kigeni waliopo Simba SC hivi sasa ni Waganda watupu, mabeki Joseph Owino aliyepoteza namba kikosi cha kwanza, Juuko Murushid na washambuliaji Emmanuel Okwi, Simon Sserunkuma na Dan Sserunkuma.
Poppe amesema kwamba Kiongera ni mchezaji wao ambaye wamemtoa kwa mkopo kwao Kenya kwa sababu alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya goti.
“Yule mchezaji bado ni mali yetu na tunaendelea kumtekelezea haki zake. Hiyo ni kwa sababu tunaamini juu ya uwezo wake wa kufunga mabao, atakuja kutusaidia,”amesema Poppe.
Ingawa Owino hana nafasi kikosi cha kwanza, lakini hata akina Sserunkuma nao hawako salama, kwa sababu hadi hivi sasa bado hawajaonyesha umuhimu wao katika timu.

![]() |
| Kiongera atarejeshwa Simba SC msimu ujao |
Poppe amesema kwamba Kiongera ni mchezaji wao ambaye wamemtoa kwa mkopo kwao Kenya kwa sababu alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya goti.
“Yule mchezaji bado ni mali yetu na tunaendelea kumtekelezea haki zake. Hiyo ni kwa sababu tunaamini juu ya uwezo wake wa kufunga mabao, atakuja kutusaidia,”amesema Poppe.
Ingawa Owino hana nafasi kikosi cha kwanza, lakini hata akina Sserunkuma nao hawako salama, kwa sababu hadi hivi sasa bado hawajaonyesha umuhimu wao katika timu.

.png)
0 comments:
Post a Comment