Na Mwandishi Wetu, MWANZA
MWANZA ni miongoni mwa mikoa nchini ambayo inaongoza kuzalisha wachezaji nyota kwa miaka mingi sasa.
Hiyo ni tangu enzi za akina Ibrahim Magongo, Khalid Bitebo ‘Zembwela’, Hussein Amaan Marsha, Mrisho Ngassa na hata sasa, Mwanza imeendelea kuzalisha nyota.
Desturi hiyo inaendelea vizuri na wadau mbalimbali wa mkoa wanaibuka na mikakati mipya kila kukicha ili kuzalisha wachezaji wa viwango vya juu zaidi.
Si lazima uwe na uwezo wa kumiliki timu ndiyo ufikirie kuzalisha na kukuza vipaji- hilo limedhihirishwa na mdau Mbaki Mutahaba, mdogo wa mmoja wa Wakurugenzi wa Clouds Media Group.
Mbaki Mutahaba ameanzisha kituo chake eneo la Bwiru mjini Mwanza, akianza na vijana wanne tu, ambao anawaandaa kuwa wachezaji bora baadaye nchini.
Mbaki amejenga nyumba maalum eneo la Bwiru ambayo wanaishi vijana hao wanne, ambao ni Ismail Khalfan, Andrea Michael wa Mwanza, Boaz Charles wa Manyoni, Singida na Paschal Kibandula wa Ifakara, Morogoro ndani yake ikiwa na gym, darasa la kupata elimu ya darasani na mahitaji mengine muhimu.
Mkuu wa kituo hicho ni Francis ‘Fura’ Felician, beki wa zamani wa Toto Africans, Pamba za Mwanza, Kagera Stars (sasa Kagera Sugar) ya Bukoba na Sony Sugar ya Kenya.
Fura anawasimamia watoto hao kuhakikisha wanatekeleza programu zote walizowekewa kuanzia za elimu na mazoezi, tena yeye akiwa ndiye kocha wao Mkuu.
Katika mahojiano na BIN ZUBEIRY wiki iliyopita mjini Mwanza, Felician mdogo wa mshambuliaji wa zamani wa Pamba ya Mwanza na Yanga SC ya Dar es Salaam, Fumo Felician anasema kwamba waliwapata watoto hao baada ya kuzunguka kusaka vipaji nchi nzima.
“Tuna vigezo fulani tulikuwa tunatazama kwa vijana, kama maumbo, uwezo, kipaji na weledi vile vile. Na kwa kuwa uwezo wetu sisi ni mdogo, kwa kuanzia, tukasema tuchukue vijana wanne tu, ila baadaye tukija kupata wafadhili tutaongeza vijana,”anasema Felician.
Mkuu huyo wa kituo hicho kinachokwenda kwa jina Football House, amesema watoto hao wanafanya mazoezi na wachezaji wa kituo cha Almasi, maarufu Almasi akademi Uwanja wa sekondari ya Bwiru.
“Tunachokifanya sisi, hawa vijana mbali ya kuwa na programu zao maalum, lakini baadaye wanachanganyika na vijana wenzao wa Almasi akademi kufanya mazoezi,”anasema.
Anasema ili kupata uzoefu, vijana hao wamesajiliwa na timu ya Almasi akademi ambayo inashiriki Ligi Daraja la Tatu ngazi ya Mkoa wa Mwanza.
Fura anasema mradi huo ulianza mwaka 2012, lakini ni mwaka jana ndipo walipokodisha hosteli na kuanza kuwatunza vijana hao na kwamba lengo lao ni kuhakikisha wanacheza Ulaya au Amerika.
“Hapa ni sehemu ya kuanzia tu, ikitokea hata timu kubwa za hapa baadaye zikavutiwa na vijana wetu kama bado hawajapata nafasi ya kwenda nje, tutawapa kwa makubaliano maalum wawatumie,”anasema Felician.
Beki huyo wa zamani wa timu ya Mkoa wa Kagera, anasema kwamba ana imani sana na mradi huo kama utazalisha matunda, ingawa wameanza nao taratibu.

![]() |
| Francis Felician nyuma ya vijana wake, kutoka kulia Boaz Charles, Paschal Kibandula, Andrea Michael na Ismail Khalfan katika Uwanja wa sekondari ya Bwiru |
![]() |
| Paschal Kibandula kushoto na Boaz Charles wakivua vifaa vyao vya michezo baada ya kurejea kutoka mazoezini |
![]() |
| Wachezaji wa Football House wanafanya mazoezi na kuchezea timu ya Almasi akademi |
Mbaki Mutahaba ameanzisha kituo chake eneo la Bwiru mjini Mwanza, akianza na vijana wanne tu, ambao anawaandaa kuwa wachezaji bora baadaye nchini.
Mbaki amejenga nyumba maalum eneo la Bwiru ambayo wanaishi vijana hao wanne, ambao ni Ismail Khalfan, Andrea Michael wa Mwanza, Boaz Charles wa Manyoni, Singida na Paschal Kibandula wa Ifakara, Morogoro ndani yake ikiwa na gym, darasa la kupata elimu ya darasani na mahitaji mengine muhimu.
Mkuu wa kituo hicho ni Francis ‘Fura’ Felician, beki wa zamani wa Toto Africans, Pamba za Mwanza, Kagera Stars (sasa Kagera Sugar) ya Bukoba na Sony Sugar ya Kenya.
Fura anawasimamia watoto hao kuhakikisha wanatekeleza programu zote walizowekewa kuanzia za elimu na mazoezi, tena yeye akiwa ndiye kocha wao Mkuu.
Katika mahojiano na BIN ZUBEIRY wiki iliyopita mjini Mwanza, Felician mdogo wa mshambuliaji wa zamani wa Pamba ya Mwanza na Yanga SC ya Dar es Salaam, Fumo Felician anasema kwamba waliwapata watoto hao baada ya kuzunguka kusaka vipaji nchi nzima.
“Tuna vigezo fulani tulikuwa tunatazama kwa vijana, kama maumbo, uwezo, kipaji na weledi vile vile. Na kwa kuwa uwezo wetu sisi ni mdogo, kwa kuanzia, tukasema tuchukue vijana wanne tu, ila baadaye tukija kupata wafadhili tutaongeza vijana,”anasema Felician.
![]() |
| Kijana Boaz Charles akiwa amelala katika hosteli yao |
![]() |
| Ismail Khalfan akisafisha vyombo jikoni katika hosteli yao |
![]() |
| Andrea Michael akifanya mazoezi katika gym iliyopo kwenye hosteli yao |
![]() |
| Darasani; Mwalimu wa sekondari ya Bwiru akimuelekeza Paschal Kibandula huku wenzake wakiendelea kujisomea |
Mkuu huyo wa kituo hicho kinachokwenda kwa jina Football House, amesema watoto hao wanafanya mazoezi na wachezaji wa kituo cha Almasi, maarufu Almasi akademi Uwanja wa sekondari ya Bwiru.
“Tunachokifanya sisi, hawa vijana mbali ya kuwa na programu zao maalum, lakini baadaye wanachanganyika na vijana wenzao wa Almasi akademi kufanya mazoezi,”anasema.
Anasema ili kupata uzoefu, vijana hao wamesajiliwa na timu ya Almasi akademi ambayo inashiriki Ligi Daraja la Tatu ngazi ya Mkoa wa Mwanza.
Fura anasema mradi huo ulianza mwaka 2012, lakini ni mwaka jana ndipo walipokodisha hosteli na kuanza kuwatunza vijana hao na kwamba lengo lao ni kuhakikisha wanacheza Ulaya au Amerika.
“Hapa ni sehemu ya kuanzia tu, ikitokea hata timu kubwa za hapa baadaye zikavutiwa na vijana wetu kama bado hawajapata nafasi ya kwenda nje, tutawapa kwa makubaliano maalum wawatumie,”anasema Felician.
Beki huyo wa zamani wa timu ya Mkoa wa Kagera, anasema kwamba ana imani sana na mradi huo kama utazalisha matunda, ingawa wameanza nao taratibu.

.png)
0 comments:
Post a Comment